Header Ads Widget

ZAIDI YA WAKAZI ELFU 34 WILAYA YA ILEMELA KUONDOKANA NA ADHA YA MAJI.

  NA CHAUSIKU SAID MATUKIO DAIMA MWANZA 

Wakazi zaidi ya elfu 34 Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza wanatarajia kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kutokana na ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa chanzo Cha maji Igombe unaendeleaje kutekelezwa.

Akizungumza baada ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa katika Wilaya hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira" (MWAUWASA) Neli Msuya ameeleza kuwa kata nne za Bugongwa, Shibula, Kahama, Nyamohongolo na maeneo jirani ndizo zitakazonufaika na mradi huo na mpaka sasa tayari mradi umeishafikia asilimia 65.

Msuya ameeleza kuwa kukamilika Kwa mradi huo utawapunguzia wakazi wa maeneo hayo adha ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji na utekelezaji wa mradi huo ni kuboresha chanzo Cha zamani ambacho kilikuwa hakizalishi maji kutokana na hali ya Ziwa.

"sasa Kwa kuboresha chanzo hichi maana yake ni kwamba tutaweza kuzalisha maji masaa 24 Kwa siku Saba zote Kwa wiki na wananchi watapata maji safi na salama na yenye uhakika" Alisema Msuya.

Kwa upande wake Mhandisi anayetekeleza ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa chanzo Cha maji Igombe Mhandisi Said Mbembela kutoka kampuni ya Equiplus Company Limited ameeleza kukamilika Kwa mradi huo utakuwa umegharimu kiasi Cha sh, Mil 585.

Hadija Kalola, na Fotunatus Joseph ni baadhi ya wakazi wa kata hizo watakaonufaika na mradi huo wameeleza kuwa changamoto walizokuwa wakipitia kabla ya kuanza kuboreshwa Kwa chanzo hicho ilipekea hadi kwenda Ziwani kutafuta maji na kwenda umbali mrefu katika chanzo kingine Cha maji.

"Kuboreshwa Kwa chanzo hichi kitatusaidia kuchota maji karibu na kuepuka kwenda umbali mrefu wa kutafuta maji, hivi sasa utakapokamilika mradi huu titakuwa tumepata maji safi na salama" Walisema.

 Miradi ya maji inayotekelezwa katika Wilaya ya Ilemela ni pamoja na Mradi wa uboreshaji wa chanzo Cha maji Igombe, Mradi wa usambazaji wa mabomba na Mradi wa ujenzi wa magati.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI