Na Matukio DaimaApp
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( TAMISEMI) Dkt, Mohamed Mchengerwa, ameupongeza uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam chini ya mkuu wake Albert Chalamila kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia miradi ya maendeleo na utekelezaji wake .
Pongezi hizo alizitoa jijini Dar es Salaam katika kongamano la wamachinga wa Kariakoo la kumpongeza Rais Dkt Samia na kuliombea Taifa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika hivi karibuni.
Amesema njia waliochagua wamachinga ndio sahihi ya kuleta maendeleo na kuisaidia Serikali inawaunga mkono ili waweze kuendelea kwani Taifa la Tanzania linaendelea kuwa salama na amani Rais wa JMT amefanya makubwa ikiwemo kuwashika wafanyabishara.
Sambamba na hayo, ametoa maelekezo Wilaya ya Ilala kuhusu ujenzi wa Jangwani Mpya na majengo ya kisasa ya Wamachinga yaweze kuongezwa katika mji wa kisasa majengo ya wafanyabishara wamachinga yawekwe eneo hilo ujenzi ukikamilika waweze kutumia masoko na wao.
Akizungumzia masoko ya mkakati yatakayojengwa mikoa yote pia wamachinga wapewe kipaumbele sekta hiyo muhimu ya wafanyabishara nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa wowote kutokana na jitihada zake za utendaji kazi katika juhudi za kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
"Katika wakuu wa wilaya wanaofanya kazi na kujituma Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo anafaa kuwa mkuu wa mkoa wowote kutokana na ufanyaji kazi wake katika kuisaidia Serikali ya Tanzania ya Dkt.Samia Suluhu Hassan ,ameweza kumsaidia Rais, ambapo pia katika wakuu wa Wilaya Tanzania Edward Mpogolo anashika namba moja anajishusha kwa jamii "alisema Waziri Mchengerwa.
Waziri Mchengerwa alisema Viongozi wa wilaya ya Ilala wanafanya kazi nzuri kwa kushirikiana pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu wamepata Mbunge makini kwa kuchapa kazi kwa maslahi ya Ilala na Taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine amemwagiza Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila aendelee kufanya kazi kwa weledi na kuakikisha Dar es Salaam inakuwa kitovu cha amani katika kipindi chote.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila alizungumzia mgogoro wa Wafanyabishara Wenye Asili ya Wachina alisema changamoto hiyo inaitaji ustarabu utumike na Demokrasia watakaa na kikao na Waziri wa Viwanda Selemani Jafo kwajili ya kumaliza mgogoro huo uliojitokeza na wafanyabishara wa Tanzania.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alimpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya chama kwa kutoa zaidi ya bilioni 300 za miradi mbali mbali ya maendeleo ya sekta ya Elimu, afya na miundombinu ya barabara.
Akizungumzia Wamachinga wa wilaya ya Ilala alisema hivi karibuni Rais atajenga soko la machinga la lisasa hivyo wafanyabishara waendelee kufurahia matunda ya Serikali yetu ya awamu ya sita
Hata hivyo, amesema mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri alisema mikopo yote itaenda kwa wafanyabishara vikundi vyote vilivyosajiliwa ambavyo vimeomba mikopo ya Serikali na kutimiza taratibu .
Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema mikakati ya Rais kila mtu afanye shughuli zake kwa Amani na mambo makubwa yanakuja ya Serikali ya Dkt.Samia ambapo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wafanyabishara Wamachinga kwa kufanya Kongamano kubwa hilo huku aliwataka wajiandae mwezi Octoba kumpigia kura Rais Dkt.Samia kwa wingi .
0 Comments