Header Ads Widget

MBUNGE GHATI CHOMETE AKIFIKIA KITUO CHA AFYA KISORYA KUTOA MSAADA WA MASHUKA


Na Shomari Binda-Bunda

WAGONJWA wanaohudumiwa kwenye kituo cha afya Kisorya kilichopo jimbo la Mwibara wilayani Bunda wamemshukuru mbunge Ghati Chomete kuwafikia na kuwafariji.

Licha ya kuwafariji ametoa msaada wa mashuka kwaajili wodi za kituo hicho zitazoweza kusaidia wagonjwa watakaolazwa kwaajili ya matibabu.

Msaada huo ameutoa leo mei 26,2025 alipofika kituoni hapo akiambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Wilaya ya Bunda.

Wakizungumza hospitalini hapo wagonjwa waliofika kupata matibabu na wale waliolazwa wamemshukuru mbunge huyo kwa moyo wake wa upendo.

Wamesema ni viongozi wachache wanaoguswa na kuwa na moyo wa kuifikia jamii kwa lengo la kusaidia na kutoa faraja.

Mmoja wa wagonjwa waliokuwa hospitalini hapo aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Suleiman mkazi wa Kisorya amesema yupo jirani na kituo hicho cha afya na hajawahi kuona kiongozi yoyote aliyekitembelea na kutuo msaada.

Amesema moyo alionao mbunge huyo ni wa pekee na anastahili kupewa shukrani na kuomba viongozi wengine waige mfano wake.

" Moyo wa mbunge huyu wa viti maalum mkoa wa Mara ni wa pekee na nimekuwa nikiona taarifa zake akifika kila mahala kusaidia jamii.

" Wabunge wa namna hii ndio tunao wataka sio mbunge anachaguliwa anapotea na anakuja kuonekana baada ya miaka mitano",amesema.

Akizungumza hospitalini hapo mbunge Ghati Chomete amesema kufika kwenye kituo hicho cha afya ni moja ya jukumu lake la kuifikia jamii.

Amesema licha ya kutoa msaada huo amefika pia kuona huduma zinazotolewa na kusikia uhitaji wa kituo hicho ili aweze kufikisha sehemu husika kwaajili ya msaada zaidi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI