Header Ads Widget

WAZIRI GWAJIMA AOMBA BUNGENI TSH BIL. 76.06 KWA AJILI YA MAJUKUMU YA WIZARA MWAKA 2025/26

Na Matukio Daima App.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amewasilisha bungeni maombi ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26, ambapo ametaja makadirio ya mapato na matumizi yanayofikia jumla ya Shilingi bilioni 76.06 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya wizara.

Akizungumza bungeni leo, Dkt. Gwajima alisema:"Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2025/26, Wizara imekadiria kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 7.04 kutoka katika vyanzo mbalimbali. Vyanzo hivyo ni pamoja na: Ada za Vyuo vya Maendeleo ya Jamii; Mitaala ya vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii; Ada ya malazi kwa wanafunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Usajili; Ada ya usajili wa wafanyabiashara ndogondogo na ada za mwaka za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali."

Akiendelea na maelezo ya matumizi, Waziri Gwajima alisema:"Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2025/26, Wizara inakadiria kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 49.12 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 26.47 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na Shilingi bilioni 22.65 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi."

Kwa upande wa miradi ya maendeleo, Dkt. Gwajima alieleza kuwa:"Mheshimiwa Spika, kwa upande wa shughuli za maendeleo, Wizara inakadiria kutumia Shilingi bilioni 26.94 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 15.42 ni Fedha za Ndani na Shilingi bilioni 11.53 ni Fedha za Nje."

"Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2025/26, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum (Fungu 53) inaomba jumla ya Shilingi bilioni 76.06 ili kutekeleza majukumu yake."

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI