Header Ads Widget

TRA MISSENYI YAPONGEZWA UKUSANYAJI WA MAPATO.

 

Na Shemsa Mussa -Matukio daima 

                 Kagera.

Mamlaka ya Mapato Tanzania,wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera imepongezwa katika ukusanyaji Bora wa Mapato huku ikiwa imavuka makisio ya ukusanyaji wa Kila Mwezi.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi wakati akifanya mazungumzo na Mwandishi wa kituo hiki,alipomtembelea Mkuu huyo katika ofisi yake kwa lengo la kujua na kifahamu miradi ya maendeleo iliyopo,Mikakati waliyonayo ya kuhakikisha  wananchi wanapata huduma zote muhimu.

Akizungumza na Mwandishi Wetu  akiwa ofisini kwake Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Hamis Maiga amesema kwa kipindi Cha Miaka miwili iliyopita Halmashauri ilikuwa inakusanya kiasi Cha Shilingi Million 600 kwa Mwezi  na kwa Sasa inakusanya takribani Billion 1.3 ndani ya Mwezi mmoja.

"Kwa kule Mutukula TRA ya Mutukula kwa kweli ufanisi wao umekuwa Mkubwa sana na wanafanya kazi kubwa Sana na kwa Mwezi huu tu wameweza kukusanya kiasi Cha Shilingi Billion 8 wamejitahidi sana,lakini na TRA ya hapa hapa ndani nao wanafanya kazi vizuri sana kwa Mwezi uliopita wameweza kukusanya asilimia takribani 600,amesema Mhe Maiga "

Pia Mkuu huyo amesema wilaya hiyo inaendelea kufanya kazi katika sekta mbali mbali ikiwemo Elimu,umeme ,Afya pamoja na Maji,amesema kwa upande wa umeme tayari vijiji vyote 77 vimefikiwa na huduma ya umeme,na kwa upande wa Maji mjini upatikanaji upo asilimia 98% na upande wa vijijini ni asilimia74%

Amesema katika suala la Elimu bado Halmashauri inajitahidi kuhakikisha inaongeza ufahulu kwa wanafunzi na mabadiliko yameanza kuonekana tofauti na Matokeo ya miaka miwili iliyopita,huku akisema katika miundombinu  Barabara zote zinapitika misimu yote katika kiangazi na masika.

"Mafanikio yote tuliyonayo hapa Missenyi  yanatokana na matumizi mazuri ya teknologia mfano kama Mapato ya TRA tunatumia mifumo mizuri na kwa upande wa Elimu walimu wanatumia vizuri vishkwambi katika kufundishia pamoja na yote hayo tuna mawasiliona mazuri na nchi jirani ya Uganda, ndio maana wilaya  Missenyi ina sura mbili za kuwa wilaya na Taifa  kwa sababu tumepakana na Taifa la Uganda ,ameongeza Mhe Maiga"

Katika upande wa kilimo Mhe Maiga amesema ili kukabiliana na changamoto za uvunaji wa  kahawa mbichi imeundwa (Task force) ambayo Wajumbe wanatoka katika idara tofauti ikiwemo Takukuru,Uhamiaji,jeshi la polisi, pamoja na wataalamu wa ushuru,ikiwa na kazi ya kutoa Elimu kwa wakulima juu ya madhara ya kuuza kahawa kabla ya wakati pamoja na bei ya zao Hilo.

"Kwa Mwaka Jana wilaya ilipewa lengo la  kukusanya kahawa tani Milion 2,tuliweza kukusanya kiasi hicho tulikusanya tani Million 2.3 na kwa kufanya hivyo Halmashauri iliongeza Mapato ,na kwa Mwaka huu tumeanza maandalizi mapema hivyo tunategemea lengo tulilopewa tutalifikia kwa asilimia zote, ameongeza Mhe Maiga "

Pia ameitaja baadhi ya miradi ya kimkakati inayotarajiwa kuanza hivi karibuni ikiwemo Mradi wa ujenzi wa soko la kisasa bunazi ambao ujenzi huo utaghalimu kiasi Cha Shilingi Billion 9 ,soko la kimataifa litakalojengwa kabakesa,upanuzi wa mwalo wa kabindi ambao utawekwa vifaa vya kisasa pamoja na ujenzi wa mnanda wa ngo'mbe katika  kata ya kakunyu.

Hata hivyo Mkuu huyo ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi Bora na mikubwa ikiwa idadi kubwa  ya miradi hiyo tayari imeanza kutumika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI