Na Shomari Binda-Matukio Daima
WATUMISHI wa umma na wananchi wamepongeza uteuzi wa Dkt. Rhimo Nyansaho kuwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Utumishi wa Umma ( PSSSF) uliofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Uteuzi wa Dkt.Nyansaho aliyekuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Azania ulifanyika jana mei 26,2025.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi na watumishi wa umma wamesema Dkt.Nyansaho anaonyesha usimamizi mzuri wa kile achokisimamia hivyo atafanya vizuri kwenye nafasi hiyo.
Wamesema kwa kupitia taasi yake ya Nyansaho Foundation amekuwa akiifikia jamii na kuisaidia na kuwa msikivu hivyo hata nafasi hiyo ataitendea haki.
Mmoja wa watumishi wa umma wilayani Serengeti ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema ana imani Dkt.Nyansaho atakwenda kufanya kazi nzuri kwenye mfuko huo wa watumishi.
Amesema uwajibikaji wa majukumu yake bila shaka ndio uliopelekea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kumuona na kumteua kwenye nafasi hiyo.
" Dkt.Nyansaho ni kiongozi makini na mtulivu atakwenda kufanya vizuri kwenye nafasi yake mpya aliyoteuliwa na mheshimiwa Rais.
" Mfuko wa PSSSF unasimamia pamoja na masrahi ya watumishi wa umma wakiwemo wastafu ni imani yetu tunakwenda kuwekewa mazingira mazuri baada ya kustafu",amesema.
Mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina Magesa Mtaka mkazi wa Natta amesema Dkt.Nyansaho ni mtendaji mzuri hivyo anakwenda kufanya makubwa kwenye mfuko wa PSSSF.
0 Comments