Header Ads Widget

WATUMISHI 621 WA NCAA WALIOKULA KIAPO KUVISHWA VYEO WASISITIZWA KUZINGATIA MAADILI YA UTENDAJI KAZI.


 Na Jusline Marco  Arusha

Jumla ya watumishi 621 wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA wakiwemo maafisa 145 na askari wa jeshi la uhifadhi 476 wamevishwa vyeo na Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka  hiyo Dkt. Elirehema Doriye leo Mei 12, 2025 na kukumbushwa kuzingatia kiapi walichoapa na kuzingatia maadili ya utendaji wa kazi,sheria, ushirikiano na upendo huku wakijiepusha na vitendo vya rushwa kwenye maeneo yao ya kazi.


Akizungumza baada ya kuwaapisha na kuwavisha vyeo watumishi hao Dkt. Doriye amewakumbusha kuwa, kupanda cheo ni kuongezewa majukumu ya kiuongozi katika usimamizi wa shughuli za uhifadhi, utalii, ulinzi, maendeleo ya jamii na urithi wa asili na utamaduni uliopo hifadhi ya Ngorongoro.

Dkt.Doriye ameongeza kwa kusisitiza kuwa suala la mafunzo ya kijeshi kwa watumishi wa NCAA litakuwa endelevu ili kuendelea kujenga utimamu wa mwili kwa afisa na askari.

Awali akizungumza katika tukio hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi (SACC) anayesimamia Idara ya Rasilimali watu na Utawala Salma Chisonga ameeleza kuwa tukio la kuvishwa vyeo kwa watumishi hao ni utekelezaji wa vibali vya kupandisha vyeo watumishi ambavyo vilitolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2021/2022 hadi mwaka 2024/2025.

SACC Chisonga amebainisha kuwa maafisa 145 waliovishwa vyeo wamegawanyika katika ngazi mbalimbali ambapo Maafisa uhifadhi Wakuu daraja la kwanza ni 5, Maafisa uhifadhi Wakuu daraja la II ni 21, Maafisa uhifadhi waandamizi ni 31, Maafisa uhifadhi daraja la I ni 56 na Mafiasa uhifadhi daraja la II ni 32.

Ameongeza kuwa askari 476 waliovishwa vyeo wamegawanyika katika ngazi mbalimbali ambapo askari wa uhifadhi mkuu daraja la I ni  39, askari wa uhifadhi wakuu daraja la II ni 54, askari wa uhifadhi Waandamizi ni 70, askari wa uhifadhi daraja la kwanza ni 86 na askari wa uhifadhi daraja la II ni 227.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI