Header Ads Widget

WAKULIMA WAITAKA SERIKALI ITOE FEDHA KATIKA KILIMO IKOLOJIA .

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo,Mifugo na Uvuvi imeombwa na wakulima wa Mikoa ya Singida na  Dodoma  kuishauri  Serikali kuweka mitaala ya kufundishia kuanzia elimu ya Msingi hadi Chuo Kikuu katika mazao ya Kahawa,Parachichi,Pamba,Viungo na Kokoa.

Wakulima wametoa kauli walipokutana na kamati hiyo bungeni Jijini kupitia Mpango mkakati wa kilimo ikolojia kupitia usimamizi wa  shirika la ActionAid Tanzania.

Akiwasilisha mapendekezo ya wakulima, Janeth Nyamayahasi  ameomba  kuweka kwa mitaala kutoka Elimu ya Msingi hadi Chuo Kikuu kama ilivyo kwa mazao ya Kahawa,Parachichi, pamba, viungo na kokoa 

"Utekelezaji wa mkataba wa Afrika Mashariki wa kilimo cha Oganiki (EAC Organic Product Standard) unaolenga kuhusanisha viwango vya ubora wa bidhaa za kilimo ikolojia tunaomba upewe kipaumbele," amesema.

Pia wameomba Serikali  kutoa ruzuku kwa pembejeo za kilimo ikolojia kama vile mbegu, mbolea na viwatilifu na kuweka ruzuku itakayowezesha wakulima kumudu gharama zaurasimishaji bidhaa za kilimo ikolojia 

Aidha, Katika wasilisho lake ameiomba Serikali kutenga fedha za ruzuku ya Kilimo ikolojia ili ziweze kuwasaidia wakulima kukopa Kwa masharti nafuu ya kurejesha kwa muda mrefu kwa ajili ya kuangalia usalama wa chakula na kugharamia mbegu za asili.

Hata hivyo mara baada ya wabunge hao kupokea mapendekezo hayo wamekiri kuwa iko haja Serikali kutenga fedha zitakazotosha kusaidia Kilimo ikolojia kutokana na hali ya mabadiliko ya tabianchi.

Mbunge wa Moshi Vijijini Profesa Aloyce  Ndakidemi amesema hali ya hewa na jinsi ardhi ilivyochoka mashambani, hakuna namna lazima wakulima wajikite zaidi kwenye kilimo ikolojia ili kuwa na uhakika wa kuvuna.

Profesa Ndakidemi ambaye ni mbobezi katika ufundishaji wa wataalamu wa kilimo, amesema nafasi ya wakulima katika kutengeneza na kuimarisha uchumi wa nchi inawezekana lakini jambo la kusisitiza ni lazima wapewe nafasi ya kueleza changamoto zao.

"Moja ya mambo ambayo nayaona Kwa wakulima wetu ni pale ambapo sisi watunga sera tunapoacha kuwasikiliza, tunawapuuza na wakati mwingine tunahisi kama hawajui kitu wakati siyo kweli," amesema Profesa Ndakidemi.

Akizungumzia suala la matumizi ya mbegu za asili amesema ni sawa lakini ingependeza kama wakulima watakuwa wakichanganya kwani baadhi ya maeneo ni muhimu wakapanda mbegu za kisasa ili kukuza kipato.

Mbunge wa Viti Maalum Kunti Majala amesema kitu kikubwa cha kuzingatia katika kilimo ikolojia ni matumizi ya mbegu kwani bila kufanya hivyo maana halisi ya ikolojia inaondoka.

Kunti ametolea mfano wa mbegu za alizeti ambazo katika msimu wa mwaka jana 2023/24 wakulima wengi walikula hasara baada ya kupanda kwani hazikuota.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI