Na Fatma Ally Matukio DaimaApp
Wakili Peter Madeleka leo amechukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kivule kupitia tiketi ya Chama cha Act Wazalendo .
Mapema leo amefika katika katika Ofisi za Chama cha Act Wazalendo zilizopo Jimbo la Kivule Kata ya Kitunda, akiwa na wafuasi wa Chama hicho kuchukua fomu hiyo na kuomba ridhaa ya Chama hicho kumpitisha kugombea Jimbo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kuchukua fomu hiyo amesema ameamua kugombea Jimbo hilo ili kuweza kuwasaidia wananchi kutokana na changamoto nyingi za kijamii zinazowakabili Jimbo humo.
"Jimbo hili ni jipya lakini hakuna maendeleo yoyote yaliyoletwa, barabara ni mbovu hazipitiki mvua zikinyesha mawasiliano yanakua shida, limesahaulika kwa muda mrefu sasa nimekuja mkombozi wao"amesema Wakili Madeleka
Amesema kuwa, miongoni mwa ajenda zake atazokwenda nazo endapo chama kitampaa ridhaa ya kugombea katika Jimbo hilo ni kusimamia haki na kuhakikisha anaweka misingi mizuri ya watu kuishi bila maumivu.
"Kila mtu ana haki ya kuishi hakutokua na matekaji wala mauwaji
leo ni siku ya kuchukua fomu wakati wa kampeni bado tutaanda siku maalum ya kukaa pamoja kama wanakivule tukajadili matatizo yetu ili mwisho wa siku tuwe na maamuzi ya pamoja ya kuikataa CCM na mawakala wake wote " amesema Wakili Peter Madeleka.
Ameongeza kuwa, Jimbo la Kivule ni miongoni mwa majimbo yanayoongoza kwa shida nchini Tanzania,hivyo kipaumbe chake cha kwanza ni kuhakikisha anaziondoa changamoto za kijamii kama barabara, maji,elimu bora Afya pamoja na kuwapatia umeme wa uhakika.
Amesema kuwa, licha ya kuwepo na changamoto nyingi kwenye uchaguzi lakini wao hawawezi kususia uchaguzi kwani wizi wa kura umekuepo muda mrefu lakini watapambana nao wakiwa pamoja, watahakikisha wanalinda kura zao ikibidi hata kulala kwenye vituo vya kumpigia kura.
0 Comments