Na Shomari Binda-Musoma
ILANI ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) ya mwaka 2025/2030 kugusa kasi ya maendeleo vijijini imemgusa mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete
Akizungumza kwa njia ya simu na Matukio Daima kutoka mkoani Dodoma baada ya kuzinduliwa kwa ilani hiyo na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema maendeleo yatazidi kufaa maeneo ya Vijijini.
Amesema maendeleo yamekuwa yakifanyika Vijijini na kutajwa kwenye ilani kufanyika kwa kasi ni jambo jema linalokwenda kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo.
Ghati amesema ilani imezungumzia kuhusiana na kufikisha umeme kila kitongoji suala linalokwenda kuinua uchumi wa wananchi kwenye maeneo yao.
Amesema umeme ni uchumi na utakapofika vitongojini zipo shughuli za kiuchumi zitakazofanywa na wananchi na kujiongezea kipato.
Mbunge huyo amesema ilani iliyozinduliwa na CCM ni bora zaidi ambayo kwa asilimia kubwa imezungumzia masuala ya maendeleo.
" Tumeona ilani moja ya mambo muhimu iliyoyazungumzia ni kasi ya maendeleo vijijini tumeipokea na itakwenda kusaidia maendeleo.
" Tunamshumkuru Mwenyekiti wa chama taifa na kamati ya ilani kuja na tiba ya maendeleo hasa kwa wananchi wetu wa maeneo ya vijijini",amesema.
Amesema iani ya CCM ya mwaka 2025/2030 imeibuka kuwa moja ya nyaraka bora zaidi za kisera kuwahi kutolewa na chama hicho tangu kuanzishwa kwake kwani Imejikita katika kuyatambua na kuyapatia majibu masuala muhimu yanayowagusa watanzania kwa kiwango kikubwa kutoka vijijini hadi mijini.
Amedai imeweka msingi imara wa maendeleo endelevu kwa kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anaishi maisha ya heshima na ustawi na imeelekeza nguvu zake katika kuboresha huduma za msingi, miundombinu, na fursa za kiuchumi kwa wote.
0 Comments