Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond akiangalia mbegu asili za wakulima
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara Kilimo na Mifugo wakiongozwa na Mwenyekiti wake Deo Mwanyika wakinunua mbegu asili kutoka kwa wakulimaMbegu asili zikiwa juu ya meza
Na Matukio Daima Media
WADAU wa mbegu asili nchini wameshauriwa kuongeza nguvu kwenye uhamasishaji na utoaji wa elimu kuhusu faida za mbegu hizo kwa wakulima ili waweze kuzitumia.
Ushauri huyo umetolewa na Mratibu wa Mtandao wa Baionuai Tanzania (TABIO), Abdallah Mkindi, hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utafiti uliofanywa na taasisi ya AFSA kuhusu faida ya mbegu za asili kwenye kilimo.
Amesema wadau wa kilimo wana kazi kubwa ya kuhakikisha mbegu asili zinatumika kwa wingi kwenye kilimo, kwa kuwa zinazalisha mazao mengi ambayo yanaimarisha afya za watumiaji.
Mkindi amesema iwapo kila mdau atakuwa anahamisha wakulima kutumia mbegu za asili ni wazi upotevu wa mbegu hizo utaanza kurejea.
"Wadau tunaWakulima wanaotumia mbegu asili wakionesha mbegu zao kazi ya kufanya kuhakikisha mbegu za asili zinasaidia katika kuimarisha afya zetu, mtindo wa maisha wa sasa umechangia mbegu hizo kutopewa kipaumbele, lakini sisi tunaendelea na jitihada za kutoa elimu na kuhamasisha kwa wakulima kuzitumia kulinda baionuai na kuimarisha afya zao,”amesema Mkindi.
Mratibu huyo amesema kilimo cha kutumia mbegu asili za wakulima ni endelevu na kinachangia utunzaji mazingira, kuhamasisha matumizi ya mbegu asili kwa wakulima kutambua na kuunga mkono mbegu zao kutoka enzi na enzi zikitumika.
Amesema katika kuhakikisha mbegu hizo zinapatikana kwa urahisi, wameanzisha zaidi ya benki 40 za mazao aina mbalimbali kulingana na uzalishaji wa eneo husika.
Mkindi amefafanua kuwa mbegu ndio nguzo kuu katika uzalishaji wa kilimo na mbegu zilizohifadhiwa na wakulima huchangia idadi kubwa ya usambazaji.
Aidha, amesema kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania na kimeweza kuajiri zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania kulingana na taarifa ya Wizara ya Kilimo (MOA 2023). Pia sekta hii inachangia wastani wa asilimia 26.6 kwa Pato la Taifa (GDP).
"Hadi sasa zaidi ya wakulima 200,000 wamejengewa uwezo wa matumizi sahihi ya mbegu asili kwa kushirikiana na mashirika zaidi ya 30 ambayo yamejikita kwenye uhamasishaji wa kilimo ikolojia hai," amesema.
Mratibu huyo amesema pamoja na kuhamasisha wakulima kujikita kwenye kilimo cha mbegu asili, pia wanaendelea kuhamasisha serikali irekebishe sheria na sera ya mbegu ambazo kwa sasa hazitambui mbegu hizo.
Pia amessma TABIO kila kukicha wanapigania mbegu asili ambazo asilimia 90 zinamilikiwa na wakulima na imani yao ni siku moja kuona wakulima wote wanatumia mbegu hizo kwani zina faida kiuchumi, afya na mazingira.
Mkindi amesema, pamoja na jitihada wanazofanya kupigania mbegu asili, pia wanaiomba serikali ifanikishe uwepo wa sheria na sera ya mbegu asili.
Mwisho
0 Comments