Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika – Tawi la Tanzania (MISA Tan) imepongeza uwasilishaji wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, iliyowasilishwa leo bungeni na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Paramagamba Kabudi, pamoja na Katibu Mkuu Bw. Gerson Msingwa.
Mwenyekiti wa MISA Tan, Bw. Edwin Soko, amesema kuwa kuongezeka kwa bajeti hiyo ni ishara njema kwa maendeleo ya shughuli za wizara, hususan katika sekta za habari, utamaduni na sanaa, ambazo ni muhimu kwa kukuza demokrasia na utamaduni wa taifa.
Bw. Soko pia ametoa wito kwa Mheshimiwa Rais kutafakari uwezekano wa kuifanya sekta ya habari kusimama kama wizara huru, badala ya kuwa chini ya wizara pana kama ilivyo sasa, ili kutoa nafasi ya kujadili kwa kina masuala ya taaluma ya habari bila kuingiliwa na sekta nyingine.
0 Comments