Header Ads Widget

UTPC, IMS, JAMIIAFRICA WAZINDUA MRADI HUU MKUBWA

Na Fatma Ally Matukio DaimaApp

Umoja wa Klab  za waandishi wa Habari Tanzania  (UTPC ), JamiiAfrica kwa kushirikiana na IMS leo wamezindua mradi wa miaka 3 unaolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za uhakika zinazohusu watu na maendeleo.

TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa kwa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Kenneth Simbaya amesema kuwa mradi huo unakwenda kusisitiza uandishi unaoweka maslahi ya wananchi mbele.

"Uandishi kama huu umekua ukikosekana ukilinganisha namna habari zinavyoandikwa sasa hivi, hivyo, huu mradi unakwenda kutukumbusha namna bora ya uandishi wa habari zilizosahihi ambazo zitakazosaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi kwa kupata habari za uhakika"amesema Kenneth 


Amesema kuwa, pamoja na mambo mengine pia mradi huo unakwenda kuwajengea uwezo kwenye uandishi wa kiusalama zaidi kwani ni muhimu Jamii kuweza kupata habari iliyokamilika .

"Umoja wa Klab za waandishi wa habari tunazo club katika mikoa yote Tanzania, hivyo club hizi zitatusaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi kupitia mradi huu"amesema 


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica Maxence Melo ameeleza mradi huo umeanza tangu 2022 ambapo 2024 ulitangazwa kutafuta washirika, huku utekelezaji wake ukiwa umeanza mapema mwaka huu .

"Mradi huu haulengi uchaguzi bali wananchi,  kipindi kama hiki waandishi wanahitaji sana kushirikishwa na sio kuwekwa kando ili waweze kuwasaidia  wananchi wafanye maamuzi sahihi "

Ameongeza kuwa, mwaka 2022 walizindua Jamii Check ambapo wameanza kuwajengea uwezo waandishi wa habari, wazalishaji wa maudhui kidigital pia watawafikia wananchi ili kuweza kutumia taarifa sahihi na kufanya utafifi kwa kushirikiana na wadau.TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

"Kwa kushirikiana na UTPC na IMS tutaandaa shirikisho la umoja wa waandishi wa habari na vyombo vya habari tuweze kuwasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi"


Nae, Imani Henrick Luvanda ni Mwandishi wa Habari kutoka Crown Medi na DW Kiswahili ni miongoni mwa watoa mada katika mradi huo ambapo amesema katika kuelekea kwenye  uchaguzi ni vyema wanahabari kupatiwa mafunzo ili kujiepusha kuingia kwenye mkumbo wa kusambaza taarifa za uongo.

Amesema kuzinduliwa kwa mradi huo utasaidia sana waandishi wa habari hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inashuhudia mabadiliko makubwa ya kidital, wanapotokea watu kama hawa wa kuwajengea uwezo ni jambo kubwa hasa kwa kipindi hiki ambapo akili mnemba imekua ikisumbua sana.

mkurugenzi wa Matukio Daima Media akipongezana na mkurugenzi wa The Chanzo baada ya uzonduzi huo 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI