Na Matukio Daima App.
Wakati mwenge wa Uhuru ukihitimisha mbio zake katika wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe na kuelekea wilayani Makete,Viongozi wa wilaya Hiyo wameagizwa kwenda kuwahamasisha wananchi waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao kwa maendeleo ya taifa huku ukiweka jiwe la msingi ujenzi wa nyumba za zaidi ya shilingi Milioni 800.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu Ismail Ali Ussi akiwa wilayani Makete katika eneo la makabidhiano amewaagiza viongozi wa wilaya ya wanging'ombe kwenda kushirikiana na wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo pamoja na kushiriki katika uchaguzi mkuu ambao ni muhimu kwa ustawi wa taifa.
Aidha mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Wanging'ombe umeweka jiwe la Msingi ujenzi wa Nyumba 7 za watumishi katika kitongoji cha Wangama kijiji cha Chalowe kata ya Igwachanya zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 800.
Hata hivyo Ismail Ali Ussi Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 amepongeza jitihada katika ujenzi wa Nyumba hizo zitakazowapa hamasa wakuu wa Idara kufanya kazi kwa bidii kutokana na kuishi katika makazi ya uhakika.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Zakaria Mwansasu wakati akikabidhi mwenge huo kwa mkuu wa Wilaya ya Makete Kissa Gwakisa Kasongwa amesema wilayani Wanging'ombe mwenge huo umeondoka kwa kufanyakazi kubwa na kupitia miradi ya zaidi ya shilingi bilioni 2.
Baada ya kumbizwa kwenye wilaya ya Makete Mwenge huo unakabidhiwa wilaya ya Ludewa ambako nako utapitia miradi mbalimbali
0 Comments