Header Ads Widget

NMB FOUNDATION IMETOA MASHINE 15 ZA KUBANGUA KOROSHO MKURANGA

Na Matukio Daima Appy.

MKURANGA.NMB Foundation imetoa mashine 15 za kubangua korosho kwa wakulima  wa zao hilo wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani zenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 4 kwa ajili ya kusaidia kuongeza thamani ya zao hilo ili wajihimarishe kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna wakati wa kufunga mafunzo ya kuongeza thamani ya zao la korosho kwa wanawake na vijana 54 wa Mkoa wa Pwani katika kiwanda cha kubangua korosho cha kikundi cha korosho wilayani Mkuranga alisema mashine hizo zitakabidhiwa ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo.


Amesema NMB FOUNDATION imekwishawezesha vikundi vya wabangua korosho 200 nchini ikiwa ni mkakati kwa kushirikiana na Rabo foundation ya nchini Uhoranzi ambapo mafunzo hayo ya wiki mbili yamefanyika kupitia mradi unaotekelezwa katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.

Mwakilishi wa bodi ya korosho Tanzania, Christopher Mwaya amesema serikali imejiwekea malengo ya kuvuna tani milioni moja kwa mwaka ambazo zitabanguliwa na kuuzwa hapa hapa nchini ifikapo mwaka 2030 ikiwa ni pamoja na kujipa jukumu la kuhamasisha ulaji wa korosho nchini li tani hizo za korosho ziuzwe hapa hapa nchini bila kutegemea soko la nje.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Omary Mwanga akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo aliwataka wahitimu hao kwenda kuitumia elimu waliyoipata kuwapa na wenzao ambao hawakufanikiwa kuhudhuria mafunzo hayo.


“Tunaishukuru sana NMB Foundation kwa kuichagua wilaya yetu kuwa mwenyeji wa mafunzo haya ambayo ni muhimu kwa wakulima wetu kwani zao la korosho thamani yake ikiongezeka na kipato cha wakulima nacho kitakuwa kikubwa,” alisema Mwanga.

Kuhusu -NMB Foundatioan ni Asasi ya Benki ya NMB inayowekeza kwenye jamii kupitia miradi mbalimbali ya Elimu, Ujasiriamali, Kilimo na Mazingira.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI