Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU KUPOKELEWA KESHO MANISPAA YA MTWARA,WANANCHI WAOMBWA KUJITOKEZA KUUPOKEA.

 


Mtwara.


Manispaa ya Mtwara Mikindani wanatarajia kuupokea mwenge wa Uhuru kesho na kutembelea katika miradi sita ndani ya manispaa hiyo.


Katika kuelekea kwenye  tukio hilo leo  Mei 24,2025 zimefanyika mbio za taratibu "Jogging" katika kuhamasisha wakazi wa Mtwara Manispaa kuweza kujitokeza katika mapokezi hayo pamoja na mkesha utakao fanyika katika viwanja vya Saba saba.



Mkurungezi wa manispaa ya Mtwara Mikindani Mwalimu Nyange amewaomba wakazi wa manispaa hiyo wajitokeze kuupokea Mwenge wa Uhuru  na kufika kwenye maeneo ambayo utatembelea.


"Niwaombe sana wananchi kujitokeza kwenye miradi tutakuwa na miradi sita.Ambao hawatakuwa kwenye msafara basi tuwakute kwenye miradi mkiwa na hamasa yakutosha.Kutakuwa na mambo mawili makubwa kwenye mkesha kwanza mkesha wa mwenge pia kutakuwa na runinga kubwa kwaajili ya kuangalia mchezo wa fainali ya shirikisho barani Afrika tukishuhudia Simba wanalibakiza kombe nyumbani"amesema Nyange mkurugenzi manispaa ya Mtwara.



Mkurugenzi ametaja baadhi ya miradi itakayo tembelewa na mwenge ambayo ni Mradi wa vijana wakufyatua tofali Ufukoni ,mradi wa maji wa Mwera,shule ya sekondari Tandika na kuweka jiwe na Msingi  zahanati ya Mtawanya.


Baadhi ya washiriki katika mbio hizo za taratibu "Jogging" wamewashukuru walio andaa na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika matukio yatakayo husisha mbio za mwenge pia wasiache kufanya mazoezi.


Mauridi Salmini amesema anawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika kuupokea mwenge wa Uhuru pia wananchi wasiache kufanya mazoezi.


"Nashukuru kwa hii jogging imetukusanya watu katika mazoezi haya wananchi wa Mtwara manispaa nawaomba tujitokeze kwa wingi katika jambo hili pia niwaombe watu kufanya mazoezi hata wakiwa majumbani na hata viongozi nao wafanye mazoezi wasituache tukifanya wananchi tu"amesema Mauridi mmoja wa washiriki wa jogging.


Mbio hizo za taratibu "Jogging" zimeungwa mkono na Shirika la Maendeleo ya Petroli na wakiwakilishwa na Marie Msellemu  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano -TPDC ambaye amesema kwao wao Mtwara ni kama nyumbani kwasababu  kunavisima vya kesi asilia.


 "Tupo Mtwara na gesi asilia ndiko inakotoka tumekuja nyumbani kutia hamasa ya mbio za mwenge wa Uhuru  ambao utakimbinzwa kesho Mtwara manispaa.Mitambo yetu ya gesi asilia ipo Madimba ambapo kunakia kikubwa tanazalisha umeme pia nishati safi ya kupikia ambayo mama Samia ndiyo kinara"amesema Msellemu.


Msellemu amesema wameamua kuungana kwapamoja na kuja kuhamasisha ili mwenge uendelee kuleta maendeleo.


"Sisi tuna clabu za oil na gess sipo 20 tunazo zilea Tumeungana kwa pamoja kuja kuhamasisha ili mwenge uendelee kuleta maendeleo." amesema Mselemu.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI