Header Ads Widget

MJUMBE KAMATI YA UTEKELEZAJI UWT AKABIDHI NONDO ROLA 20

 


Na  Matukio Daima Media

Mbeya 

MJUMBE  wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT ya CCM Wilaya ya Mbeya ,Hobokela Mwankina amekabidhi Nondo Rola 20 ,Kwa ajili ya umaliziaji wa Nyumba ya Mtumishi ya Jumuiya hiyo iliyopo kata ya Iwindi.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Hobokela Mwankina ambaye ni mjumbe wa Kamati ya utekelezaji UWT wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya amesema kuwa lengo la uchangiaji huo ni utekelezaji wa ilani chama hicho ya uchaguzi mkuu 2020.

 "Hii ni sehemu  ya kuongeza ushiriki wa jamii katika shughuli za Maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi (Katibu UWT Wilaya ya Mbeya Vijijini)"amesema Mwankina.

Amesema kuwa kama Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT ya  CCM Willaya  ana wajibu kushiriki shughuli za maendeleo kama hizi ni sehemu ya jukumu langu hivyo msukumo ni kutekeleza majukumu ya UWT .

Aidha Mwankina amesema kwamba kushiriki shughuli za maendeleo za UWT ni takwa lake ambalo anapaswa kulifanya katika kutekeleza majukumu ya umoja huo .

Hata hivyo amesema kuwa kinapotokeza kitu chochote cha kutelekeza katika umoja huo hakuna budi kufanya ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI