Header Ads Widget

MATHIAS CANAL ACHANGIA VIFAA VYA MICHEZO SHULE MBILI ZA MSINGI IRAMBA//AMPA HEKO DKT MWIGULU NCHEMBA



NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Mshindi wa Tuzo za SAMIA KALAMU AWARDS na Afisa Mtendaji Mkuu wa WAZOHURU MEDIA Ndg Mathias Canal amechangia vifaa vya michezo katika shule mbili za Msingi ambazo ni Kiomboi Bomani na Kiomboi Hospitali.

Vifaa hivyo amevikabidhi kwa Wakuu wa Shule hizo mbili ikiwemo Jezi jozi mbili za mpira wa miguu kwa kila shule, jezi jozi mbili za mpira wa pete, mipira kwa ajili ya mchezo wa Pete na mchezo wa mpira wa miguu.



Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo tarehe 17 Mei 2025 katika shule ya msingi Kiomboi Bomani na kuhudhuriwa na Diwani wa kata ya Kiomboi Mhe Omary Omary, Afisa Elimu kata ya Kiomboi Mwl Fabiana Mbuta, Wakuu wa shule, na walimu wakiwemo walimu wa michezo, Mathias amesema kuwa vifaa hivyo vya michezo vitakuwa chachu ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wanafunzi sambamba na kuwaweka pamoja wanafunzi ili kutojiepusha na makundi ovu.

Pia, Mathias ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Iramba kuendelea kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mhe Mwigulu Mchemba ili aweze kutekeleza kwa ufasaha majukumu yake katika Taifa la Tanzania.


Mathias amempongeza Dkt Mwigulu kwa kushirikiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda kwa kuongeza bajeti ya wizara kutoka Trilioni 1.9 mwaka 2024/2025 hadi kufikia shilingi Trilioni 2.4 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo kuna ongezeko la zaidi ya shulingi Bilioni 500.


Kadhalika, Mathias ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha walimu kujiandikisha kwenye Daftari la mpiga kura ili waweze kuyumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua ama kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu.

Kwa nyakati tofauti Diwani wa Kata ya Kiomboi Mhe Omary Omary, Mwl Sadick Mkoma, Mwl Lulu Shayo, Mwl Dorocus Mungulu, Leonard Mayombo, Emanuel Nalaila na Afisa Elimu kata ya Kiomboi wamempongeza Mathias Canal kwa kuendelea kujitolea kwa kukumbuka shule aliyosoma na kuona haja ya kurudi nyumbani kufanya maendeleo kwa ajili ya jamii yake.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI