Waziri wa madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde(Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa bodi ya taasisi ya watoa huduma katika sekta ya madini(TAMISA).
Taasisi hiyo mpya ya TAMISA inaundwa na watanzania walioungana na wadau wengine ikiwa na lengo la kutoa huduma katika sekta ya madini nchini .
Peter Andrew mwenyekiti wa taasisi hiyo ya TAMISA ,amesema kuwa ujio wa taasisi hiyo umekuja kuunganisha wadau wote na makampuni yanayotoa huduma katika sekta ya madini kuwa taasisi moja.
"TAMISA imeanzishwa ikiwa na lengo la kuwa taasisi moja, wito wetu kwa watanzania, wajasiriamali na wenye makampuni yanayotoa huduma za madini kujiunga na TAMISA kwaajili ya kuunganisha nguvu zetu pamoja."
Sebastian Ndege ambae ni mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano TAMISA, nae amebainisha kuwa umoja wa taasisi hiyo utajadili kwa pamoja masuala muhimu katika sekta ya madini huku ikiendelea kuhabarisha kuhusu fursa za uwekezaji pamoja na kuunganisha nguvu ya wadau wa sekta hiyo.
Uzinduzi wa bodi ya taasisi hiyo unatarajiwa kufanyika, mei 16 jijini Dar es salaam hafla itakayohudhuriwa na Waziri wa madini pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka sekta ya madini.
0 Comments