Na Fadhili Abdallah, Kigoma
Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa amesema kuwa mapenzi ya Rais Samia kwa mkoa Kigoma yapo moyoni na ndiyo sababu kubwa iliyofanya mkoa huo kuletewa kiasi cha Trilioni 12 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo yaa wananchi.
Katimba alisema kuwa mapenzi hayo ya Rais Samia yanatokana na mapenzi makubwa ambayo wananchi hao wameyaonyesha kwa Raisi huyo wa nchi ikiwemo ushindi mkubwa ambao mkoa Kigoma imeupatia Chama Cha Mapinduzi wakati wa mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Naibu Waziri huyo wa TAMISEMI alisema hayo akizungumza na vionngozi wa CCM wa mkoa Kigoma, wilaya Kigoma, mabalozi, viongozi wa kata na matawi wa manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo viongozi Zaidi ya 1300 walihudhuria mkutano huo.
Katika Mkutano huo Naibu Waziri huyo wa TAMISEMI alisema kuwa Rais Samia aliahidi kuufungua mkoa Kigoma kiuchumi na biashara na kwamba jambo hilo limeonekana kutekelezwa kwa vitendo ambapo fedha hizo zimetekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha miundo mbinu ya aina zote ambayo imekuwa kichocheo kwenye uchumi na biashara kwa mkoa huo na nchii kwa jumla.
Awali Katibu wa CCM mkoa Kigoma,Christopher Pallangyo alisema kuwa chama kimechukua nafasi yake katika kuisemea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ikiwemo uboreshaji wa miradi ya miundo mbinu, miradi ya afya, elimu na miradi yote ambayo inagusa maisha ya wananchi.
Pallangyo alisema kuwa ili kuisemea miradi hiyo alisema kuwa walifanya ziara ya mabalozi wote wa manispaa ya Kigoma Ujiji kutembelea miradi ya uboreshaji wa bandari, ujenzi wa meli mpya, ukarabati wa meli ya Mv.Liemba na Mt.Sangara, uboreshaji uwanja wa ndege wa Kigoma, mradi wa umeme wa gridi ya taifa na miradi ya elimu na afya ili waweze kuijua kwa undani.
Baada ya kutembelea miradi hiyo Katibu huyo wa CCM mkoa Kigoma amemuomba Naibu Waziri huyo kusaidia na kuwezesha mabalozi hao wa manispaa ya Kigoma Ujiji kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya treni ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma ambayo serikali imetoa Zaidi ya trilioni sita ambapo itawezesha wajumbe hao kuujua kwa undani mradi huo.
Mwisho
0 Comments