Header Ads Widget

KIJANA BODABODA ANAYESHITAKIWA KUWA KUUA MTOTO WAKE KWA KUMKATA VIPANDE KISHA KUMTUPA CHOONI IRINGA AFIKISHWA MAHAKAMANI

 

Na Matukio Daima Media ,Iringa

Kijana dereva bodaboda eneo la Lukosi kata ya Mkwawa mjini Iringa Joseph Muhulila (28) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumuua mtoto wake kwa kumkata vipandevipande na kutupa mwili wake chooni .

Mshitakiwa huyu alifikishwa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Iringa leo  majira ya saa 6 mchana chini ya ulinzi mkali wa polisi .

katika kesi hiyo ya mauaji ya kukusudia namba 11594/2025 inayomkabili Dereva huyu Bodaboda anatuhumiwa kumuua mtoto wake Timotheo Muhulila (6) kisha kumkatakata vipande na kumtumbukiza chooni .

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Rehema Mayagilo mshitakiwa huyu alisomewa shitaka moja la mauaji ya kukusudia alilolifanya Aprili 11, 2025.

kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo akiwa mtaa wa Lukosi kata ya Mkwawa mjini Iringa kwa kumuua kwa Timotheo Muhulila (6) kwa kukusudia kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Mwendesha mashtaka upande wa jamhuri wakili mwandamizi Radhia Njovu alisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.



Hata hivyo Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kile kwani Mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo hivyo Joseph Muhulila amerudishwa tena rumande hadi Mei 28, 2025 kutokana na shauri hilo kukosa dhamana kama ilivyoelekezwa katika kifungu cha 148 (5) (a) (I) sura namba 20 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai.


TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI