Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Kigoma kimezidi kupata pigo la kuondokewa na viongozi na wanachama wake baada ya viongozi wa wilaya ya Kakonko na kata 19 katika wilaya hiyo kujivua uanachama katika chama hicho na kujiunga na Chama Cha ACT Wazalendo.
Viongozi na wanachama hao walijivua uanchama wa CHADEMA mbele ya kiongozi mstaafu wa chama hicho, Zitto Kabwe wakiongozwa na aliyekuwa Katibu wa CHADEMA jimbo la Kakonko mkoani Kigoma, Filbert Protas.
Akizungumza baada ya baada ya kujivua uanchama aliyekuwa Katibu wa CHADEMA jimbo la Kakonko, Filbert Protas kwa niaba ya viongozi na wanachama wa CHADEMA waliojivua uanchama na alisema kuwa wameamua kuachana na CHADEMA na kujiunga na ACT Wazalendo baada ya kuona viongozi wa chama hicho wanadhamiria ya kupigania maslahi yao binafsi badala ya wanachama wao na wananchi kwa jumla.
Protas alisema kuwa amefanya kazi CHADEMA jimbo la Kakonko kwa miaka 28 ikiwemo kufanikisha chama hicho kushinda nafasi ya ubunge mwaka 2015 lakini kwa sasa hayafanyiki na chaama kimejaa vurugu na mambo ya ubinafsi hivyo wameamua kujiunga na ACT Wazalendo kwa kuwa imeonyesha nia ya dhati ya kupigania maslahi ya umma.
Akizungumza baada ya kuwapokea viongozi na wanachama hao wa zamani wa CHADEMA kiongozi Mstaafu wa ACT wazalendo,Zitto Kabwe alisema kuwa alipokea maombi ya viongozi hao kujiunga na chama hicho kwa hiari yao wakiwa na nia ya kurudisha nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya upinzani katika uchaguzi mkuu ujao badala ya kuwaachia CCM wafanye wanavyotaka kufanya.
Zitto alisema kuwa tafiti mbalimbali walizofanya zinathibitisha kwamba sehemu kubwa ya wapiga kura katika chaguzi zilizopita na uchaguzi ujao wanatoka upinzani hivyo wakati huu wamedhamiria kuwatumia wapiga kura wao kuhakikisha wanawachagua viongozi wa chama hicho kwa ngazi mbalimbali.
“Tunaingia kwenye uchaguzi tukiwa na wajibu wa kuikabili CCM kwenye sanduku la kura hatutasubiri huruma maana tunajua mbinu zao walizofanya kwenye chaguzi mbili zilizopita hivyo wakati huu tumedhamiria kuifanya ACT Walendo kushinda nafasi za Ubunge na udiwani nchi nzima,”Alisema Zitto.
Mwisho.
0 Comments