Header Ads Widget

ZELENSKY NA TRUMP WAKUTANA KABLA YA MAZIKO YA PAPA

 

Zelensky (wanne kutoka kushoto) na Trump (wa tatu kutoka kulia) wakisimama wakati jeneza la Papa likipitishwa kwa ajili ya ibada ya maziko Vatican

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na Rais wa Marekani, Donald Trump, wamekutana Roma kabla ya maziko ya Papa Francis Vatican.

Maafisa kutoka pande zote mbili wamethibitisha mkutano huo ulifanyika, huku Ikulu ya White House ikiuelezea kuwa "wenye tija sana". Hakuna maelezo zaidi kuhusu mazungumzo hayo yaliyotolewa.

Trump na Zelensky wanahudhuria ibada hiyo katika Jiji la Vatican pamoja na wakuu wengine wa nchi na wanafamilia za kifalme, akiwemo Prince William, Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer, na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Mkutano wao unakuja siku moja baada ya Trump kusema Urusi na Ukraine "wako karibu sana kufikia makubaliano", kufuatia mazungumzo kati ya mjumbe wake Steve Witkoff na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow siku ya Ijumaa.

Mkutano huo ulikuwa ziara ya nne kama hiyo ambayo Witkoff amefanya nchini Urusi tangu kuanza kwa mwaka, na mazungumzo hayo ya saa tatu baadaye yalielezewa kuwa "yenye manufaa sana" na msaidizi wa Putin, Yuri Ushakov.

Ushakov pia aliongeza kuwa yameleta "misimamo ya Urusi na Marekani karibu zaidi, si tu kuhusu Ukraine bali pia kuhusu masuala mengine ya kimataifa" ambapo "uwezekano wa kuanzisha tena mazungumzo ya moja kwa moja kati ya wawakilishi wa Urusi na Ukraine ulijadiliwa haswa".

Steven Cheung, mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu ya White House, alisema maelezo zaidi kuhusu mkutano wa faragha wa Jumamosi kati ya Trump na Zelensky yatatolewa.

Viongozi hao walikwaruzana na kurushiana maneno katika mkutano wao Ukilu ya Maerekani, na haikutarajiwa wangekutana ana kwa ana katika wiki za karibuni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI