Header Ads Widget

ANDENGENYE: MUUNGANO UMEWAFANYA WATANZANIA KUWA WAMOJA

 

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amesema kuwa kuendelea kuwepo kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kielelezo kikubwa cha kuonyesha umoja na mshikamano wa Watanzania bila kujali tofauti za dini wala kabila.

Andengene alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye soko la Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji na soko la Mwandiga halmashauri ya wilaya Kigoma  mikutano iliyotanguliwa na  zoezi la usafi kwenye maeneo hayo akiongoza watendeji wa serikali na wananchi wa maeneo hayo.

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Kigoma,Rashid Chuachua alisema kuwa maahimisho ya miaka 61 ya Muungano inadhihirisha ukomavu wa Watanzania katika kuvumilia hivyo kuhakikisha Amani na usalama wa nchii vinapewa kipaumbele katika kila jambo ikiwemo masuala ya kisiasa.



Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa asilimia 90 ya watu waliohudhuria maadhimisho hayo ya miaka 61 ya Muungano mkoani Kigoma wamezaliwa ndani ya Muungano ambao hadi sasa umeifanya nchi kuwa na Amani hivyo kuomba kila mmoja kwa nafasi yake anahakikisha analinda na kuienzi Amani ya nchi kupitia tunu hiyo ya Muungano.

Awali akitoa salamu kwenye maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama Cha CHAUMA mkoa Kigoma, Abdallah Bukuku alisema kuwa maadhimisho hayo ya miaka 61 ya Muungano yanapaswa kuwa somo kubwa namna nchi inavyotekeleza majukumu yake kwa Amani ukilinganisha na nchi zote za jirani hasa zile za ukanda wa maziwa makuu ambazo zinakabiliwa na   mapigano ya ndani ya wenyewe kwa wenyewe hivyo kuhimiza Amani ya nchi ilindwe kwa nguvu zote.




Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mwandiga (CCM),Angel Kebero amepongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine waliomtangulia kwa kuona umuhimu wa uwepo wa muungano huo na kuitaka serikali kutokubali wasaliti kuingia kati na kusababisha muungano huo kuvunjika.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI