Header Ads Widget

"MIAKA 61 YA MUUNGANO ZANZIBAR INAKANDAMIZWA" - OTHMAN

 Na mwandishi wetu Zanzibar.

Wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 61 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa  Othman Masoud Othman amesema ipo  haja ya kufanyika kwa mabadikiko mkubwa ya mfumo wa Muungano  ili Nchi zote mbili za washirika  zipate haki sawa.

Othman ameyasema hayo leo April 26 katika ukumbi wa Samael Chakechake Pemba alipokua akizungumza na maelfu ya vijana wa Chama hicho katika kongamano maalumu la maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano.

Alisema uwepo wa Muungano huu kwa muda mrefu unaikandamiza Zanzibar licha ya kuwa na rasilimali zake nyingi inashindwa kupata maendeleo na kukuza uchumi kama Nchi huru.

Alisema pamoja na uwepo wa  kasoro nyingi za Muungo na kulalamikiwa, watawala wanashindwa kujali  na wamekua wakiongeza mambo mengine  mapya kujinufaisha na familia zao.

"Tulianza kulalamimia mambo 11 ya Muungano hapo awali lakini sasa  tunalalamikia mambo 41 bila wenzetu kujali lolote huku mambo yote hayo yakinufaisha upande wa pili wa Tanzania Bara" alisema.

Aidha Othman ambae pia ni Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar amesema kwa nyakati tofauti viongozi mbali mbali wamekua wakifanya jitidaha kumaliza, changamoto hizo lakini hakuna mafanikio ambayo yanapatikana kwa sababu wenye nguvu ndio wenye maslahi.

"Zimeundwa zaidi ya kamati 10 kushughulikia kero za Muungano lakini zote zimeishia njiani na hakuna kilichotimia hadi leo na ndio maana tunasema wenzetu hawana ukweli" alisema.

Sambamba na hilo alisisitiza changamoto hizo zinaiathiri zaidi Zanzibar ikiwemo kukosa mamlaka ya kukopa nje ya Nchi fedha ambazo zingeweza kuendesha miradi na kukuza uchumi wa Zanzibar.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho  Ismail Jussa amesema Muungano wa Zanzibar na Tanganyika umekua na vikwazo vingi,kwa muda mrefu ambavyo viongozi mbali mbali wamekua wakivisemea.

Alisema vikwazo hivyo ni pamoja na kukoseka Kwa usawa na  Nchi zote mbili za washiriki ambazo kabla kuundwa kwa Muungano huo zilikua Nchi huru.

"Nyinyi vijana wakati tunaadhimisha miaka 61 hii ya Muungano ni lazima mufahamu vita hii haikuanza leo na nyinyi muna wajibu wa kuendeleza mpaka tutakapoleta heshima ya Zanzibar kuwa Nchi huru yenye haki na usawa katika Muungano huu.

Sambamba na hayo Jussa alisema watawala waliilazimisha Zanzibar kuingia kwenye Muungano bila ya wahusika kurusika.

Akitoa salam za vijana  Makamu Mwenyekiti Ngome ya vijana Taifa wa Chama hicho Nassor Ahmed Marhoun alisema vijana  wapo tayari kuendelea kupambana kwa njia za kidemokrasia.

Alisema njia pekee ya kuzifanya Zanzibar kupinga hatua zaidi za kimaendeleo ni lazima washirikiane kwa pamoja kuiondoa CCM madarakati katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI