Na Shomari Binda-Matukio Daima-Mara
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto Biteko amewaliza waombolezaji waliojitokeza kwenye maziko ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania ( Tanesco) Mhandisi Boniphace Gissima Nyamo-Hanga.
akitoa salamu za rambirambi huku akibubujikwa na machozi amesema Mhandisi Boniphace Gissima Nyamo-Hanga atakumbukwa kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya Tanesco.
Amesema Gissima alikuwa akijibu na kutekeleza kazi zake kwa heshima na kuheshimu teuzi zake na kufanya kazi kwa bidii.
Naibu Waziri Mkuu amesema marehemu Gissima atakumbukwa kwa unyenyekevu wake katika kuhubiri umoja na unyenyekevu kwa watumishi walio chini yake.
Amesema historia ya Mhandisi Nyamo-Hanga itaendelea kukumbukwa na Taifa kwenye suala la umeme na kuwapa pole familia na wote waliofanya nae kazi na kusema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anawapa pole na anayo hazina ya vijana na ataona nani amuweke kwenye nafasi hiyo kwaajili ya kuendeleza pale alipoishia.
" Ndugu zangu huu msiba mkubwa na Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan anawapa pole sana kufuatia msiba huu kwa kuwa Mhandisi Nyamo-Hanga alikuwa hazina kwa taifa.
" Niwape pia salamu za pole familia, wafanyakazi wa Tanesco, wana Mara kwa kumpoteza mtu muhimu kwenu na hii ni mipango ya Mungu tuwe wavumilivu kwenye kipindi hiki kigumu',amesema.
Awali akisoma wasifu wa marehemu Mkurugenzi wa Mahusiano wa Tanesco Irene Guwelo amesema Mhandisi Boniphace Gissima Nyamo-Hanga alisimamia kwa ufanisi mkubwa katika upatikanaji wa umeme vijijini na mijini,upanuzi wa mitandao ya usambazaji,usimamizi wa miradi mikubwa ya nishati na kuimalisha ushirikiano kimataifa.
Amesema katika sekta ya umeme uongozi wake aliakisi maadili ya haki,uwazi na uwajibikaji sifa zilizompatia heshima kubwa ndani na nje ya nchi.
Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi akitoa salamu za rambirambi amesema Mhandisi Nyamo-Hanga alikuwa ana mchango mkubwa kwa taifa na mkoa wake wa Mara.
Amesema kwenye safari yake ya kuja mkoani Mara moja ya kazi Ali,okuwa akija kuzifanya ni pamoja na kukagua na kuona namna ya kufikisha umeme kwenye shule ya Amali inayojengwa wilayani Butiama.
Akiendesha ibada ya maziko hayo Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi mkoani Mara John Mwita amesema kifo ni mipango ya Mungu na kila mmoja anapaswa kutenda mema kwenye jamii na kuzungumzwa vizuri atakapoondoka duniani.
Msemaji wa familia Mwita Gachuma ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa( NEC) ameishukuru serikali chini ya Wizara ya Nishati kwa kusimamia na kuratibu shughuli zote tangu kutokea kwa msiba huo aprili 13,2025. kwa ajali ya gari
Wananchi na viongozi mbalimbali wameshiriki maxiko hayo yaliyofanyika eneo la Migungani wilayani Bunda mkoani Mara
0 Comments