Header Ads Widget

MAJINA YA WASHINDI WA TUZO YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU HAWA HAPA


Na. Andrew Chale, Dar.

MAJINA ya Washindi 12 wa nafasi ya kwanza, pili na Tatu na majina ya walioingia nafasi ya 10 bora walioshinda tuzo za Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu zilizofanyika usiku wa Aprili 13, 2025.

Washindi hao 12 wametoka katika nyanja nne za Ushairi, Riwaya, Tamthilia na Hadithi za Watoto ambazo waandishi bunifu walipeleka kazi zao kushindanishwa.

Upande wa Riwaya:

Mshindi wa kwanza ni Maundu Mwingizi kutoka Dar Es Salaam, kupitia muswada wake wa "Jeneza la Taifa".

Mshindi wa pili, Majaliwa Sued, kutoka Manyara, "Kuokoka".

Mshindi wa tatu, Lucas Lubango kutoka Mwanza, "Bweni la Wavulana".

Washindi wengine walioingia Nne hadi 10 ni:

Dkt. Abbas Mohamed Omar kutoka Zanzibar "Zawadi ya Simu Janja", (8), 

Ahmad Simba Mwaita kutoka Tanga " Taifa Jipya" , (10), 

George Michael Lauwo kutoka Kilimanjaro, "Damu Nzito", (4),

Ibrahim Jaffar Mkamba kutoka Dar Es Salaam "Mashahidi kutoka Kuzimu", (7),

Philipo Oyoo Oyaro wa Mwanza: "Kwa Udi na Uvumba", (5),

Richard Mziray wa Dar Es Salaam: "Mlezi wa Vizazi" (6),

Zakaria Henry Riwa wa Dar Es Salaam: "Kilicho Chetu".(9).



Upande wa Mkusanyiko wa Mashairi /Utenzi:

Adil Ali Mwinyiae Dodoma: "Yunge", (2)

Ally Mchanyato wa Dar "Tuzo ya Usomaji", (3),

Ally Juma Isuka Dar: "Nikifa Msinizike", (5), Bakari Jecha Makame: Zanzibar: " Diwani ya Tafakuri", (8),

Hussein Kondo Abdallah wa Dar: "Diwani ya Urathi wa Mjumu" (1).

Kombo Abdalla Omar wa Zanzibar: "Kisima cha Giningi", (4),

Mbaruku Ally Mohammed wa Tanga: "Utenzi wa Nana Mkombozi", (10),

Peter Gervas Komba wa Songea Ruvuma: "Mashairi ya Maisha",(6), 

Saidi Mokiwa Ramadhani wa Tanga: "Pendo la Mama Kiboko"(7),

Sharifa Khamis Mussa wa Zanzibar: "Pambazuko" (9).





Upande wa Hadithi za Watoto:

Corona Kimaro Cermak kutoka Jamhuri ya Czech: " Tembo Zimamoto", (7),

Hafidh Ali Makame wa Zanzibar: "Siafu na Majimoto", (6),

Lilian Simon Mbaga w Dar: "Hatma Yangu",(4),

Mwanacha Mohamed Omar wa Zanzibar : "Mwisho wa Dharau" (5),

Wengine ni:

Paulina Barnabas Lugabulila wa Dar Es Salaam: "Dirisha la Ajabu",(3),

Shifaa Feisal-Amin wa Zanzibar: "Ibuni Maua na Mji wa Maweni", (2)

Tune Shaaban Salim wa Dar Es Salaam: "Maziwa ya Kuku" (1).


 Upande wa Tamthilia ni:

Ally Nassoro Ngagesa: "Kijarida",(7),

 Bupe Anthony Kabute: "Anne na Anelisa",(4),

David Shalali Shaba: "Beti ya Mauti", (10),

Elizabeth Godwin Mahenge: "Pambana" Dar es salaam(5)

Wengine ni:

Faraji Odilo Manoni kutoka Kilimanjaro: "Kovu la Maisha", (8),

Ignas Dennis Mkindi kutoka Dar: "Mwale wa Matumaini", (3),

Murungi Raeli Katabarula kutoka Kagera: "Zaidi ya Majirani", (6),

Said Yussuf Kileo kutoka Dar Es Salaam: "Mwangaza", (2),

 Sajida Salehe Athumani wa Dar: "Mwangaza wa Mvita" (9), 

Tyatawelu Emmanuel Kingu wa Dar: " Alama ya Kuzaliwa".(1)


Awali katika utoaji wa tuzo hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Profesa Penina Mlama alisema jumla ya miswada bunifu 282 ilipokelewa kutoka nyanja zote.

Profesa Mlama alisema kamati imefurahi kuona mwitikio mkubwa wa waandishi bunifu kushiriki katika tuzo hizo tofauti na mwaka jana 2024 ambapo kamati ilipokea miswada 209 na miswada 283 iliyopokelewa mwaka 2023 wakati ilipoanzishwa tuzo hizo.

“Kati ya miswada 282 iliyowasilishwa mwaka huu, ya ushairi ilikuwa 114, riwaya 46, hadhiti za watoto 77 na tamthiliya ni 45.

“Hata hivyo kwa mwaka huu jumla ya miswada iliyotimiza vigezo vilivyowekwa ilikuwa ni 205 kati ya 282, naendelea kuwasihi sana waandishi bunifu kuzingatia vigezo vilivyowekwa ili kuepuka kuwasilisha kazi ambazo hazijazingatia vigezo, washiriki wa mwaka huu wametoka katika mikoa yote ya Tanzania na miswada minne imetoka kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi,” alisema Profesa Mlama.

Kuhusu ushiriki wa wanawake kwenye tuzo hiyo, alisema walikuwa 88 sawa na aslimia 32 na kwamba hilo ni ongezeko kutoka washiriki 62 mwaka jana huku idadi ya wanaume ikiwa 194 ikilinganishwa na 155 wa mwaka jana.

Profesa Mlama aliendelea kutoa wito kwa washiriki wa tuzo hiyo kuongeza ubunifu na kuzingatia vigezo ili kupata kazi bora zaidi zenye ushindani mkubwa.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI