Na Shomari Binda-Bunda
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amezungumzia namna alivyofanya kazk na marehemu Mhandisi Boniphace Gissima Nyamo-Hanga wakati akiwa Waziri wa Nishati na Madini.
Akitoa salamu za rambirambi leo aprili 16,2025 wakati wa maziko yake yaliyofanyika eneo la Migungani wilayani Bunda amesema Taifa limepoteza kijana ambaye mchango wake bado ulikuwa ukihitajika.
Amesema afanya kazi na Mhandisi Nyamo-Hanga mwaka 2012 na alikuwa msikivu na kupokea maelekezo hasa kwenye suala la kasi ya kupeleka umeme vijijini na kupata mafanikio yanayotajwa leo kwenye suala la umeme.
Muhongo amesema kila mara alikuwa akijitisha vikao kuitisha vikao vya kuuliza namna bora ya kupeleka umeme vijijini ili wananchi wapate nishati hiyo.
Mbunge huyo amesema kazi nzuri iliyofanyika kwenye eneo hilo ilipelekea dunia kutambua kazi nzuri iliyofanywa na kutaka kutambua njia gani iliyotumika maka kufanikiwa.
Amesema kupunguza gharama za umeme na kuweka gharama nafuu ya umeme kupeleka kwa wananchi ni moja ya eneo ambalo walilisimamia vizuri wakiwa na Mhandisi Nyamo-Hanga.
" Hadi hivi sasa nilikuwa nikishirikiana na Mhandisi Nyamo-Hanga na kila nnapopata mambo huko duniani ya masuala ya umeme nimekuwa nikiwasilisna nae yeye akitekeleza hapa nchini nami nikishughulikia ya Afrika.
"Naibu Waziri Mkuu unayo timu nzuri nzuri ya vijana tumempoteza ndugu yetu lakini ni imani haya ni mipango ya Mungu tumuombee mapumziko mema",amesema
Amesema Taifa halipo nafasi mbaya kwenye suala umeme na kuomba nili kumuenzi lazima matumizi ya umeme yaongezeke barani Afrika na kufika mwaka 2030 watanzania watumie uniti 500 za umeme.
Katika hutuba yake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto Biteko amesema Marehemu Mhandisi Boniphace Gissima Nyamo-Hanga atakumbukwa kwa unyenyekevu wake wakati wote alipokuwa akitekeleza majukumu yake.
Amesema Gissima alikuwa akijibu na kutekeleza kazi zake kwa heshima na kuheshimu kila mmoja bila kujali yupo chini au juu yake.
Akiendesha ibada ya mazishi Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mara John Mwita amesema kigo ni mipango ya Mungu na kumuombea pumziko lililo jema Mhandisi Nyamo-Hanga.
Mhandisi Boniphace Gissima Nyamo-Hanga alizaliwa septemba 10,1969 na alifariki aprili 13,2025 kwa ajali ya gari na kuzikwa leo aprili 16,2025.
0 Comments