Na Shomari Binda-Musoma
WAVUVI wawili kati ya wanne waliozama ziwa Victoria usiku wa aprili 21,2025 bado hawajapà tikana licha ya juhudi za kuwatafuta.
Akizungumza kwa njia ya simu na Matukio Daima mmiliki wa mtumbwi waliozama nao wavuvi hao waliokuwa wakimfanyia kazi Silas Adam Maingu ameiomba serikali kusaidia kuwataguta wavuvi hao.
Amesema kama watu waliokuwa wakimfanyia kazi za uvuvi amefanya juhudi za kuwatafuta kwa kushirikiana na familia na jamii bila mafanikio.
Silas amesema wavuvi hao walizama siku hiyo ya aprili 21 majira ya usiku walipokuwa wakiendelea na shughuli zao za uvuvi kwenye Kisiwa cha Rukuba.
Amesema kati ya wavuvi hao mmoja alinusulika aliyemtaja kwa jina la Makebe Nyarubamba aliyepatikana akiwa amekufa maji ni Revocatus Mtega Pulizo na ambao hadi sasa hawajapatikana ni Fedrick Matiku na Cleophace Bahati Mganga
Silas anayejishughulisha na shughuli hizo za uvuvi katika Kisiwa cha Rukuba amewaomba wanaojishughulisha na uvuvi na kutumia ziwa Victoria kutoa taarifa watakapoona miili ya wavuvi hao kwa kuwa wanaweza kuonekana tofauti na walipozamia.
" Tunaendelea na juhudi za kuwatafuta ndugu zetu waliozama ziwa Victoria usiku wa aprili 21 Kisiwa cha Rukubwa wakiwa kwenye majukumu ya kazi.
" Tunaiba serikali pia itisaidie lakini pia tu.awaomba wanaotumia uvuvi ziwa watakapofanikiwa kulma miili yao maeneo yoyote watufahamishe",amesema. Silas.
Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mara Mrakibu Augustine Magere amesema wamefanikiwa kumpata mtu mmoja siku ya jana na jitihada za kuwarafuta wengine wawili bado zinaendelea.
Amesema kutokana na jografia na upepo juhudi zinaendelea kwa kushirikiana na watumiaji wengine wa ziwa Victoria wakiwemo wavuvi.
0 Comments