Header Ads Widget

MBUNGE CHEGE ATOA SHUKRANI ZIARA YA BALOZI DKT.NCHIMBI RORYA

 


NA Shomari Binda-Matukio Daima

MBUNGE wa Jimbo la Rorya Jafari Wambura Chege amemshukuru Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt.Emanuel Nchimbi kwa ziara yake kwenye jimbo hilo.


Akizungumza na Matukio Daima kwa njia ya simu leo aprili 27,2025 amesema ziara hiyo ilikuwa ni muhimu kwao.

Amesema kipekee kwa niaba ya wananchi wa Rorya kwa upendo mkubwa wanashukuru kuwatembelea na kukazia ujenzi wa barabara ya Utegi Shirati kwenda Kirongwe kwa ujenzi wa kiwango cha lami.

 Chege amesema barabara hiyo ni muhimu sana kiuchumi, kibiashara na hata ukuaji wa pato la Taifa kwa serikali pale itakapo kamilika.

Amesema kuwa na ɓarabara nzuri na inayopitika wakati wote itasaidia shughuli za kiuchumi na kuwanufaisha wananchi.

"Kwa unyenyekevu mkubwa sana tunamshukuru  Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kuendelea kusambaza upendo kwa watanzania hasa sisi Rorya na mara nyingine tena kukubali barabara hii kutangazwa na kuanza ujenzi wa kiwango cha lami kwa hatua ya kwanza ya ujenzi wa kilometa 27.

Kwa niaba ya wa watu wa Rorya tunamshukuru pia Katibu Mkuu wetu Dkt.Emanuel Nchimbi kwa kuitembelea Wilaya ya Rorya na mkoa mzima kiujumla",amesema.

Amesema wema ulipwa kwa wema hivyo wananchi wa Rorya na mkoa wa Mara wapo tayari kumchagua Rais Dkt.Samia  na Dkt. Nchimbi kwa kura za mwaka huu ili kulipa wema kwa mazuri aliyowafanyia kwa historia ya toka Rorya kuanzishwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI