Header Ads Widget

SEKI KASUGA : RAIS DKT. SAMIA AMEKIHESHIMISHA CHAMA, USHINDI NI WA KISHINDO



Seki Boniventure KasugaMjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Iringa

Na Matukio Daima Media 

Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Iringa,Seki Boniventure Kasuga  amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kukiheshimisha na kukijenga Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kasi kubwa, hali ambayo imeimarisha matumaini ya ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza na katika mahojiano yake na mwandishi wa habari hizi  Seki Kasuka  alisema kuwa kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia katika kusukuma maendeleo ya taifa ni alama ya wazi inayothibitisha dhamira ya kweli ya kuwatumikia Watanzania wote bila ubaguzi wa vyama. Alisisitiza kuwa ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu hautakuwa wa kawaida bali wa kishindo kikubwa.


Kasuga  alitaja miradi mikubwa ya kimkakati iliyotekelezwa chini ya uongozi wa Dkt. Samia kuwa ndiyo nyenzo ya msingi iliyojenga imani mpya kwa wananchi. Alisema miradi hiyo imeweka alama zisizofutika katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

 "Tunaona ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, mradi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere (JNHPP), upanuzi wa bandari zetu, ujenzi wa barabara za kiwango cha juu, hospitali za kisasa, pamoja na kuimarisha sekta ya elimu na maji," alisema Kasuga 

Kasuga alibainisha kuwa miradi hiyo ni ukombozi kwa kila Mtanzania, bila kujali anatoka chama gani. 

Alieleza kuwa maendeleo yanayoletwa na serikali ya awamu ya sita ni jibu la kiu ya muda mrefu ya Watanzania wote kutaka maisha bora na fursa za maendeleo. 

Alisema kuwa hata wale waliokuwa wakipinga kwa maneno, sasa hawana pa kuficha kwani maendeleo hayo yanajieleza yenyewe kwa vitendo.

"Hii miradi si ya CCM pekee, ni ya Watanzania wote. Hatuwezi kuruhusu watu wachache kudharau au kubeza juhudi hizi kubwa ambazo zimeleta matumaini mapya kwa kila mmoja wetu," alisema kwa msisitizo.

Kasuga  alitoa wito kwa wapinzani kuacha kubeza maendeleo na badala yake wajiunge katika juhudi za kulijenga taifa.

Akizungumzia uchaguzi mkuu ujao, Kasuga alisema kuwa zawadi pekee kwa Rais Samia na timu nzima ya CCM ni kupewa kura za kishindo.

Hata hivyo  alisema kura hizo zitakuwa ni uthibitisho wa shukrani ya Watanzania kwa kazi nzuri ya serikali na kwa matarajio makubwa ya maendeleo endelevu.

"Uchaguzi mkuu si wa kujaribu jaribu. Ni wakati wa kumwongezea Rais wetu muda wa kuendelea na kazi nzuri aliyoianza.

 Wabunge na madiwani wa CCM wanapaswa kuchaguliwa kwa wingi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo bila vikwazo," aliongeza Kasuga 

Aliwaomba  wanachama wa CCM kuendelea kueneza habari njema za maendeleo na mafanikio ya serikali ya Dkt. Samia katika kila kona ya nchi. 

Alisisitiza umuhimu wa kuwa na kampeni za amani, zenye kujenga hoja na kuhamasisha umoja wa kitaifa. 

"Tunatakiwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kushajihisha umoja, mshikamano na upendo miongoni mwa Watanzania wote, bila kujali itikadi zao," alisema.

Kasuga  alihitimisha kwa kumpongeza Rais Samia kwa ujasiri wake, hekima, na maono makubwa ya kuliongoza taifa. 


Alisema kuwa kupitia uongozi wake, Tanzania imepata heshima kubwa kimataifa na kuvutia wawekezaji wengi, hali ambayo imefungua fursa mpya za ajira kwa vijana na kuongeza pato la taifa.

"Mama Samia ameonesha kuwa ana nia ya dhati ya kuona kila Mtanzania ananufaika na matunda ya uhuru wetu. 

Kuwa kura za kishindo kwa Rais Samia, wabunge na madiwani wa CCM ni zawadi sahihi ya kuunga mkono juhudi hizi," alihitimisha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI