Header Ads Widget

WATU ZAIDI YA 83,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA PANGANI KIBAHA MJINI.

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA KIBAHA

WATU zaidi ya 83,000 wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji wa Pangani kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha Mkoani Pwani baada ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kumkabidhi mkandarasi eneo la utekelezaji wa mradi.


Aidha mradi huo utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 8.9 mara utakapokamilika na unatekelezwa na Mkandarasi wa kampuni ya Shanxi Construction Engineering Corporation and Mineral Company ya China ambapo kutakuwa na hatua tatu za ujenzi wa pampu mbili, tenki la maji na usambazaji wa maji.


Akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Pangani Kaimu Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema kuwa mradi huo ni wa miezi 12.


Mtindasi amesema kuwa mradi huo utahusisha ujenzi wa matenki mawili ambapo pampu itakuwa na uwezo wa kuzalisha lita 250,000 kwa saa ambapo yatajengwa eneo la Shirika la Elimu Kibaha (KEC).


Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Shangwe Twamala amesema kuwa wanamshukuru Rais kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya kukabili changamoto ya maji kwenye Kata ya Pangani na maeneo mengine.


Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amesema kuwa anaomba mkandarasi atekeleze mradi huo kwa wakati ili wananchi wapate huduma hiyo muhimu.


Diwani wa Kata ya Pangani Agustino Mdachi amesema kuwa wananchi walikuwa wanalia sana lakini sasa wanafutwa machozi kwa mradi huo kuanza.


mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI