Header Ads Widget

WANAFUNZI KIGOMA WAFUNGUKA UJENZI SHULE MAALUM ZA WASICHANA

 

George Mkuchika Waziri wa nchii ofisi ya Raisi Ikulu kazi maalum.

Na Fadhili Abdallah, Kigoma


WANAFUNZI wasichana wanaosoma shule ya sekondari ya Wasichana Kigoma iliyopo wilaya ya Uvinza mkoani wameipongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa shule maalum za wasichana nchini kwani zitawezesha kutimiza lengo la kuinua ufaulu wa wanafunzi wasichana katika masomo ya sayansi na kuongeza idadi ya wataalam wanawake nchini.

Wanafunzi hao wametoa kauli hiyo mbele ya Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Ikulu kazi maalum alipofanya ziara kutembelea na kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari ya WAsichana Kigoma iliyopo wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo wanafunzi hao wamempongeza Raisi Samia kwa kazi kubwa na nzuri ambayo serikali yake imefanya kwenye ujenzi wa shule hizo.

Wanafunzi hao walisema kuwa shule hiyo imejengwa ikitimiza matakwa na mahitaji ya wanafunzi katika kupata elimu hasa wale wa masomo ya sayansi hivyo wanaamini watatimiza malengo yao katika kupata elimu sambamba na kuzingatia mahitaji ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Akizungumza na jumuia ya wanafunzi wa shule hiyo, Waziri wa nchii ofisi ya Raisi Ikulu Kazi maalum, George Mkuchika alisema kuwa serikali imeliangalia suala la historia ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kike na hivyo kuja na mpango wa ujenzi wa shule maalum za masomo ya sayansi kwa wasichana ikiwemo hiyo ya Kigoma Girls Sekondari na kuwataka wanafunzi hao kuzingatia masomo ili kutimiza malengo ya serikali katika kuinua ufaulu wa wanafunzi wasichana.

Doroth Deogratius Mwanafunzi mwenye mahitaji maalum wa kidato cha kwanza wa shule ya Sekondari Maalum ya wasichana Kigoma

Veronia Masele Mwanafunzi wa kidato cha tano wa Shule ya Sekondari maalum ya Wasichana Kigoma iliyopo wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma

Majengo ya shule ya Sekondari Maalum ya Wasichana Kigoma iliyopo wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI