Header Ads Widget

HII HAPA ORODHA TEULE YA WANAOWANIA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU - 2025


Na. Andrew Chale, Matukio Daima App, Dar Es Salaam.

MWENYEKITI, Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya uandishi Bunifu, Prof. Penina Oniviel Mlama ametangaza rasmi orodha teule ya waliopendekezwa kufikiriwa kuwania tuzo hiyo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu 2025.

Orodha hiyo imetangazwa rasmi Aprili 7, 2025 mbele ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof. Adolf Mkenda, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba na jopo la majaji wa tuzo hiyo ambao mwaka huu ni msimu wa tatu.

Katika orodha hiyo, Prof. Penina amebainisha kuwa katika miswada iliyotumwa, hao waliopatikana ndo imeonekana Bora katika kuingia kwenye nafasi na kuelekea kwenye kilele cha fainali ya utoaji wa tuzo Aprili 13, katika ukumbi wa Super Dome Masaki, Dar Es Salaam.

"Majina haya 10 kila kipengele tumeyaweka kuzingatia herufi za majina ya washiriki. Hivyo haina maana kuwa namba moja ndo mshindi hapana, ifahamike hivyo, amesema Prof. Penina.

Nakuongeza kuwq, Zawadi kwa washindi mwaka huu utaratibu utabaki kama ilivyokuwa miaka iliyopita yaani:

"Mshindi wa kwanza Shilingi milioni 10. Muswada wake utachapishwa na Serikali na kusambazwa shuleni na maktaba za taifa, lakini pia atapata Ngao na Cheti.

Mshindi wa Pili Shilingi milioni 7 na Cheti. Mshindi wa tatu. Shilingi milioni 5 na Cheti. Wengine wa Nne hadi wa10 wao watapata Cheti pekee.


Majina na mikoa waliotoka na maina ya miswada yao:

Orodha hiyo ni pamoja na Riwaya:

Dkt. Abbas Mohamed Omar kutoka Zanzibar "Zawadi ya Simu Janja",  Ahmad Simba Mwaita kutoka Tanga "Taifa Jipya" ,

George Michael Lauwo kutoka Kilimanjaro, "Damu Nzito", Ibrahim Jaffar Mkamba kutoka Dar Es Salaam "Mashahidi kutoka Kuzimu", Lucas Gervas Lubango kutoka Mwanza: "Bweni la Wavulana". Majaliwa Ibrahim Sued wa Manyara: "Kuokoka".

Wengine ni:

Maundu Moris Mwingizi wa Dar Es Salaam: "Jeneza la Taifa", Philipo Oyoo Oyaro  wa Mwanza: "Kwa Udi na Uvumba", Richard Mziray wa Dar Es Salaam: "Mlezi wa Vizazi" na Zakaria Henry Riwa wa Dar Es Salaam: "Kilicho Chetu".

Upande wa Mkusanyiko wa Mashairi /Utenzi:

Adil Ali Mwinyiae Dodoma: "Yunge", Ally Bakari wa Dar Es Salaam: "Mchanyato Tuzo ya Usomaji", Ally Juma Isuka Dar: "Nikifa Msinizike", Bakari Jecha Makame kutoka Zanzibar: "Diwani ya Tafakuri", Hussein Kondo Abdallah wa Dar: "Diwani ya Urathi wa Mjumu".

Kombo Abdalla Omar wa Zanzibar: "Kisima cha Giningi", Mbaruku Ally Mohammed wa Tanga: "Utenzi wa Nana Mkombozi", Peter Gervas Komba wa Songea Ruvuma: "Mashairi ya Maisha", Saidi Mokiwa Ramadhani wa Tanga: "Pendo la Mama Kiboko" na Sharifa Khamis Mussa wa Zanzibar: "Pambazuko".

Upande wa Hadithi za Watoto:

Corona Kimaro Cermak kutoka Jamhuri ya Czech: " Tembo Zimamoto", Hafidh Ali Makame wa Zanzibar: "Siafu na Majimoto", Lilian Simon Mbaga w Dar: "Hatma Yangu", Mwanacha Mohamed Omar wa Zanzibar : "Mwisho wa Dharau".

Wengine ni:

Paulina Barnabas Lugabulila wa Dar Es Salaam: "Dirisha la Ajabu", Shifaa Feisal-Amin wa Zanzibar: "Ibuni Maua na Mji wa Maweni", Tune Shaaban Salim wa Dar Es Salaam: "Maziwa ya Kuku".

Upande wa Tamthilia ni:

Ally Nassoro Ngagesa: "Kijarida", Bupe Anthony Kabute: "Anne na Anelisa", David Shalali Shaba: "Beti ya Mauti", Elizabeth Godwin Mahenge: "Pambana" (kutoka Dar es salaam).

Wengine ni:

Faraji Odilo Manoni kutoka Kilimanjaro: "Kovu la Maisha", Ignas Dennis Mkindi kutoka Dar: "Mwale wa Matumaini", Murungi Raeli Katabarula kutoka Kagera: "Zaidi ya Majirani", Said Yussuf Kileo kutoka Dar Es Salaam: "Mwangaza", Sajida Salehe Athumani wa Dar: "Mwangaza wa Mvita" na Tyatawelu Emmanuel Kingu wa Dar: "Alama ya Kuzaliwa".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI