Header Ads Widget

WAZIRI MKUU MSTAAFU, MHE.KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI MBIO ZA MAC D MARATHON2026, APIGA KURA TUZO ZA WTA

Mgeni Rasmi katika Mbio za Riadha za MAC D Marathon ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Kassim Majaliwa akipewa maelezo ya jinsi ya kupigia kura wa vivutio vya Tanzania katika Tuzo za Utalii Duniani (World Travel Awards) kutoka kwa Afisa Utalii Lusajo Nsweve wa TAWA, Julai 4,2026, Kunduchi, Jijini Dar es Salaam.

 

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mhe. Kassim Majaliwa ameshiriki katika Mbio za Riadha za MAC D Marathon zilizofanyika Julai 4, 2026 Kunduchi, Dar es salaam.

Mhe. Majaliwa alikuwa mgeni rasmi katika Mbio hizo zenye lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupitia zenye kaulimbiu ya "Go Green with Gas" na kuunga mkono juhudi za Serikali katika utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi.

Ambapo alipata fursa kuelekezwa jinsi ya kupigia kura vivutio vya Tanzania katika Tuzo za Utalii Duniani (World Travel Awards) kutoka kwa Afisa Utalii Lusajo Nsweve wa Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Pia viongozi wengine mbalimbali wameweza kushiriki zoezi hilo,

TAWA imetumia jukwaa hilo kutangaza vivutio vya utalii inavyovisimamia pamoja na kuhamasisha zoezi la upigaji kura wa tuzo za Utalii Duniani (World Travel Awards) kwa Viongozi wa Serikali na washiriki mbalimbali.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI