Header Ads Widget

TET YAJIVUNIA TUZO ZA MWALIMU NYERERE, VITABU NAKALA 140, 000 VIMECHAPISHWA NA KUSAMBAZWA NCHINI KUTOKA KWA WASHINDI WA 2022/23

 


SERIKALI imechapisha vitabu nakala 140,000 vyenye thamani ya shilingi milioni 400 na kupeleka katika maktaba za shule za msingi Tanzania Bara na Zanzibar .

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba wakati wa zoezi la kutangaza orodha ya majina ya waliopitisha kuwania tuzo za Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Aprili 7,2025.

Ambapo amesema kwamba  vitabu hivyo vimetokana miswada ya washindi wa kwanza wa Tuzo ya Mwalimu Nyerere za Uandishi Bunifu ya mwaka 2022/23.

“Vitabu hivi vimeshambazwa shule zote kwa uwiano wa shule moja kwa vitabu 14 na kwamba wanafunzi tayari wanaendelea kuvitumia ”amesema Dkt. Komba . 

Dkt. Komba amesema kuwa Tuzo hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya uchapishaji, ambapo kila mwaka mchapishaji mmoja huchaguliwa kwa ajili ya kuchapisha vitabu vya washindi.

Katika hatua nyingine, Dkt.Komba ameeleza kuwa maandalizi ya hafla ya Tuzo ya mwaka 2025 yanaendelea vizuri ambapo itafanyika tarehe 13/4/2025 jijini Dar es salaam.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI