Header Ads Widget

WAHITIMU KIDATO CHA NNE WAITWA KUBADILISHA MACHAGUO YA TAHASUSI

 

Na Hamida Ramadhan, Mtukio Daima App Dodoma

SERIKALI imewaita wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2024 kuhusu kubadilisha machaguo ya Tahasusi za Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati na Elimu ya Ufundi kwenye mfumo wa kielektroniki wa uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Tano na Vyuo.


Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohammed  Mchengerwa, ameyasema hayo leo  jijini wakati akizungumza na waandishi wa habari Kuhusu wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2024 kufanya mabadiliko ya Tahasusi za kidato cha tano na kozi za vyuo kwa njia ya mtandao kwenye mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha tano na vyuo mwaka 2025

 Amesema hatua hiyo ni maandalizi ya awali ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga Kidato cha Tano na Vyuo vya Serikali Mwaka, 2025. 

"Itakumbukwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa fursa kwa wahitimu wa Kidato cha Nne kufanya mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (combination) na Kozi mbalimbali walizozichagua kupitia Fomu ya Uchaguzi (Selform.), " Amesema 


Na kuongeza "Fursa hii huwawezesha wanafunzi kurekebisha machaguo yao kulingana na ufaulu waliopata kwenye matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)," Amesema Waziri Mchengerwa.



Amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais  TAMISEMI imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzidata taarifa zilizo kwenye Fomu za Uchaguzi za wanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa shuleni. 


"Kukamilika kwa zoezi hili kunatoa fursa kwa wanafunzi kuweza kufanya mabadiliko ya machaguo/ tahasusi/ kozi kwa njia ya mtandao (online)," Amesema . 


Na kulngeza "Baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao, kanzidata hiyo ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia nafasi za Kidato cha Tano na Kozi mbalimbali katika Vyuo vya Kati na vya Elimu ya Ufundi kwa kuzingatia sifa za ufaulu na machaguo yao," Amesema . 


Aidha amesema Ofisi ya Rais  TAMISEMI inatoa fursa kwa wahitimu wa elimu ya sekondari Kidato cha Nne, mwaka 2024 kubadili machaguo yao ili kutoa nafasi zaidi kwa mwanafunzi kusoma tahasusi au kozi itakayomwandaa kuwa na utaalamu stahiki katika maisha yake ya baadaye.


"Hii ni kutokana na ukweli kwamba wakati wa ujazaji wa fomu za machaguo ya awali, Zoezi hili litatoa fursa zaidi ya wanafunzi kuongeza machaguo na kufanya machaguo mapya ya Tahasusi na Kozi, " Amesema 


Na kyongeza "Napenda kuwasihi wazazi/ walezi kushiriki katika zoezi hili kwa kushauriana na watoto wao katika kufanya machaguo sahihi kulingana na ufaulu wao," Amesema . 



Amesema Kwa umuhimu huo, wahitimu wote wanahimizwa kufanya marekebisho ya machaguo ya tahasusi na kozi kulingana na ufaulu wao, kwa kuingia kwenye Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) unaopatikana kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz.


 Aidha, maelekezo kwa wahitimu na jinsi ya kufanya mabadiliko watayapata kwenye mfumo kupitia user manual pamoja na video ya youtube zilizopo kwenye mfumo huo. 


Ili kuingia kwenye mfumo itabidi mhitimu atumie Namba ya Mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2024, Jina lake la Mwisho, Mwaka wa Kuzaliwa na Alama ya Ufaulu aliyopata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote atakaloulizwa.


"Ni matumaini yangu kuwa wahitimu wote watatumia kwa ukamilifu fursa waliyopewa ya kubadilisha Tahasusi na Kozi kulingana na ufaulu waliopata. Pia wataweza kusoma tahasusi/kozi ambazo wamefaulu vizuri ama wana malengo nazo zaidi," Amesema. 



Zoezi la kubadilisha tahasusi na vyuo litaanza rasmi tarehe 31 Machi, 2025 hadi tarehe 30 Aprili, 2025. Wanafunzi, wazazi na walezi wanakumbushwa kushauriana kikamilifu ikiwa ni pamoja na kupata ushauri wa kitaalam na kitaaluma kabla ya kufanya mabadiliko ya tahasusi au Kozi. 


"Ninawasisitiza wanafunzi, wazazi/ walezi kutumia muda huo vyema ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa. ," 


Na kuongeza "Ni muhimu kuzingatia muda uliotolewa wa kufanya marekebisho ili ratiba ya kuwachagua na kuwapangia shule na vyuo iweze kuendelea kwa muda uliopangwa," Amesema 


Ameekeza Baada ya matokeo ya kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa, Ofisi haitashughulikia changamoto hizo kwa kuwa fursa ya kufanya mabadiliko hayo imeshatolewa.


Huduma hii ya kubadilisha tahasusi ni bure na endapo wanafunzi watapata changamoto, wawasiliane na Dawati la Huduma la Mteja kupitia barua pepe: huduma@tamisemi.go.tz au kuwasiliana moja kwa moja na Kituo cha Huduma kwa Wateja kwa simu +255 262 160 210 na +255 735 160 210.


Aidha, pamoja na maelekezo hayo, kwa mwanafunzi, mzazi/mlezi atakayekuwa na suala linalohitaji maelezo au ufafanuzi zaidi aende katika Ofisi za Elimu za Mikoa na Halmashauri.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI