Na Habari na Matukio App
Makamu Rais DKT Philip Mpango amewataka wakimbiza mwenge wa uhuru mwaka 2025 Kitaifa Kuhakikisha wanafichua vitendo vyote vya ubadhilifu wa fedha za serikali, Rushwa na dhuruma katika mambo yote watakayo yabaini katika miradi ya halmashauri watakayo ipitia katika mbio za Mwenge nchi nzima.
Amesema hayo wakati akihutubia Wananchi katika sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa huko katika viwanja vya Shirika la elimu Kibaha wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Amesema wakimbiza Mwenge hao wa Uhuru mwaka 2025 wakafichue vitendo vyote vya ubadhilifu wa fedha za serikali, vitendo vya rushwa, udhalimu na dhuruma kwa Wananchi katika mikoa 31 na Halmshauri 195 nchini.
Makamu pia amezigiza halmashauri kuwapa ushirikiano wakimbiza mwenge hao wasifiche kuhusu matumizi ya fedha katika miradi ya serikali ilipo kwenye maeneo yao.
Waziri Mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kassimu majali amemshukuru Rais Samia kwa ridhia mbio za mwenge wa uhuru kutumika kuhamisha na kutoa elimu wananchi kujitokeza kupiga kura kwa utulivu na amani
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Vijana, ajira na watu wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete amemshukuru Rais kwa kumuamini na kusema mbio za Mwenge wa uhuru zimekuwa kichocheo cha kuendeleza mapambano ya maadui watatu wa ujinga, umasikini, malazi na vitendo vya rushwa.
Amesema wakimbiza Mwenge wa mwaka huu wataendelea kueleza historia ya nchi yetu na kueleza jamii kuhusu fedha mbalimbali zilizotolewa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa miradi ya maendeleo nchini.
Upande wake mkuu wa mkoa Pwani Abubakari kunenge pia amemshukuru Rais kuwapa fursa ya mwenge wa uhuru Kitaifa kuzinduliwa Mkoa Pwani ambao umekuwa ni chanzo cha kupata fursa mbalimbali za kiuchumi.
Naye Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani Seka Hurio amesema bank ya NMB imekuwa Mdhamini Mkuu wa shughuli za maandalizi na uzinduzi wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka huu ambayo imechangia zaidi ya shilingi Milioni 30 ikiwa ni kutoa ushirikiano kwa Wananchi ambao sehemu kubwa ni wateja wa banki hiyo.
Aidha Seka amewataka Wananchi kuachana na mikopo umiza wajiunge na Banki hiyo ambayo inatoa mikopo kuanzia shilingi 1 hadi shilingi Milioni moja bila kujaza fomu wala kuwa na.dhamana yoyote.
++++
0 Comments