Header Ads Widget

UVCCM BARIADI WASISITIZWA KUJIKITA KWENYE MASUALA YA KIJAMII.

Katibu wa UVCCM wilayani hiyo, Hussein Kimu (katikati) akipokelewa na vijana wa Kata ya Kilalo alipokwenda kufunga kongamano la UVCCM kata hiyo.



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu wametakiwa kujadili masuala yanayohusu jamii badala ya kujikita kwenye masuala yao binafsi ambayo hayana tija kwa mustakabali wa Taifa.


Aidha wametakiwa kushiriki kwenye Matukio ya kijamii na kisiasa ikiwemo kujitokeza kuwania nafasi za uongozi huku wakionywa kutotumika kisiasa kwa baadhi ya Wagombea kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.


Hayo yamebainishwa jana na Katibu wa UVCCM wilayani hiyo, Hussein Kimu wakati akifunga Makongamano ya vijana yaliyofanyika katika kata za Ikungulyabashashi na Kilalo wilayani humo yaliyolenga kutoa Elimu na kutambua fursa zinazowazunguka.


Hussein amewataka vijana hao kujikita kwenye  masuala yanayohusu Jamii ikiwemo maandalizi ya Uchaguzi Mkuu lakini pia wajikite kutangaza mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Suluhu Hassan.


"Tunakae vikao vya kujadili masuala yanayohusu jamii kwa sababu na sisi ni sehemu ya jamii, tujadili maandalizi ya Uchaguzi sababu ni sehemu ya masuala ya jamii...Mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi, CCM imeshapitisha Mgombea ambaye ni Dk. Samia, hatuna ajenda sababu kampeni tumemaliza" amesema Kimu na kuongeza.


"Kilichobaki ni kuyasema mazuri yaliyofanywa na Rais Samia, tukumbuke Maendeleo ni hatua, tumejenga Shule, Zahanati, Umeme lakini bado kuna mapungufu na changamoto ndogondogo, hizo zitatatuliwa sababu ndio hatua za Maendeleo."


Katibu huyo amewataka Vijana kujitokeza kuchukua fomu nafasi za uongozi sababu hakuna mwenye miliki ya Uongozi ndani ya Chama Chama Mapinduzi.


Amewataka vijana hao kuacha kutumika kisiasa pia kubadilika na kujitambua kuelekea kipindi cha Uchaguzi huku akiwasisitiza kuwalinda viongozi wa CCM hasa Rais Dk. Samia.


Katika hatua nyingine, Kimu amewataka vijana kujifunza Siasa na Uchumi ili waweze kujitegemea ikizingatiwa kuwa CCM imeelekeza kuwa Viongozi wa kuchaguliwa lazima wawe na kipato chao halali.


Awali Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Ikungulyabashashi, Pastori Bukanu amewataka vijana kuhakikisha wanasimamia Uadilifu, Uwajibikaji na kutenda haki katika jamii.


"Vijana tunatakiwa tusimamie uwajibikaji, na kujituma, tutasimamia vijana wapate Elimu ili wajikwamue kupitia Mikopo ya 10%, vijana tuchangamkie fursa zinazotolewa na Halmashauri sababu Kuna milikopo mingi inatengwa na na serikali na vijana tunashindwa kuchangamkia kutokana kukosa Elimu." Amesema.


Katibu wa UVCCM kata ya Kilalo, Phales Paulo amesema kutokana na elimu waliyoipata kwenye kongamano hilo wataitumia na kuchangamkia fursa kwa kubisha hodi ili kupata Mikopo ya asilimia 10 kwenye Halmashauri.


Naye Rehema Soteri, mkazi wa Kilalo amewataka vijana kujikita kwenye masuala muhimu ya kimaendeleo badala ya kufanya shughuli zisizokuwa na tija ikiwemo michezo ya kubahatisha.


Mwisho.


Katibu wa UVCCM wilayani hiyo, Hussein Kimu akiongea kwenye Mkutano wa hadhara wa Kongamano la Vijana uliofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kilalo A.




Katibu wa UVCCM wilayani hiyo, Hussein Kimu (katikati) akipokelewa na UVCCM kata ya Ikungulyabashashi alipokwenda kufunga kongamano la Vijana.






















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI