Header Ads Widget

DIWANI KIGOMA AIPONGEZA KUWASA KUMTUA MAMA NDOO

           

 Chanzo cha maji cha Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kigoma Ujiji (KUWASA) kinachotumika kusambaza maji kwa wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji 

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

 Diwani wa kata ya Bangwe Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma Hamisi Betese ameipongeza Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kwa kutekeleza mradi mkubwa wa maji kwa ufanisi ambao umewezesha kutekelezwa kwa vitendo mpango wa serikali wa kumtua mama ndoo kwenye kata hiyo.

 

Betese alisema hayo kwenye mkutano wa hadhara akieleza mafanikio makubwa ambayo kata yake imeyapata kwa miaka mitano ambayo amekuwa diwani kwenye kata hiyo ya Bangwe.

Diwani huyo alisema kuwa mwaka 2020 alipoingia madarakani kata hiyo ilikuwa inapata maji chini ya asilimia 40 jambo ambalo lilifanya idadi kubwa ya watu kwenda ziwa Tanganyika umbali wa kilometa nne kufuata huduma ya maji wakati chanzo cha maji kipo kwenye kata hiyo ambapo kwa sasa jambo hilo ni historian a maji yanapatikana kwa Zaidi ya asilimia 90.

Sambamba na hilo Betese alisema kuwa miaka mitano aliyokuwa maradakani serikali imeweza kutekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa kwenye shule za msingi na sekondari ambapo madaras 22 yenye thamani ya Zaidi ya milioni 800 yamejengwa pamoja na ujenzi wa barabara zikiwamo za lami zenye mataa.

Baadhi ya wananchi wanaoishi kata ya Bangwe akiwemo Lista Balegeya alisema kuwa kazi kubwa imefanywa na serikali kupitia KUWASA na kuweza kumaliza tatizo la maji kabisa kwenye kata hiyo ambayo kwa sasa kuna idadi kubwa ya nyumba za kisasa zinajengwa lakini maji ilikuwa tatizo kubwa ambapo kwa sasa tatizo hilo limekwisha.


Akieleza upatikanaji wa maji katika kata hiyo ya Bangwe Kaimu Mkurugenzi usambazaji maji KUWASA, Mhandisi Fransico Makoye alisema kuwa katika kata hiyo mamlaka imeweza kutambaza mtandao wa maji kwa urefi wa Kilometa 21 sambamba na kujenga tank0 lenye uwezo wa kuhifadhi  lita 300,000.

Makoye alisema kuwa utekelezaji huo ni sehemu ya mradi mkubwa wenye gharama ya shilingi Bilioni 42 ambao unawezesha mamlaka kuzalisha lita milioni 42 kwa siku katika chanzo cha maji kilichopo kata ya  Bangwe na kwa sasa upatikanaji wa maji kwa manispaa ya Kigoma Ujiji ni Zaidi ya asilimi 90.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI