Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema Muungano wa Ulaya unaandaa hatua za kukabiliana na ushuru wa Trump - akisema kwamba Ulaya "tayari iko katika harakati za kukamilisha kifurushi chake cha kwanza dhidi ya ushuru wa chuma," na kuandaa hatua zaidi za kukabiliana ikiwa mazungumzo yatashindwa.
"Ninajua kuwa wengi wenu mnahisi kukatishwa tamaa na mshirika wetu mkuu," alisema.
"Lazima tujiandae na athari zitakazoletwa na tatizo hili." Akifunga taarifa yake, von der Leyen alisisitiza msimamo wa Ulaya.
"Sisi [Ulaya] tuko katika hili pamoja: ikiwa unachukua mmoja wetu, unatuchukua sisi sote," von der Leyen alisema. "Umoja wetu ndio nguvu yetu."
Alisisitiza kuwa Ulaya "itasimama pamoja na wale walioathiriwa moja kwa moja", baada ya kubainisha hapo awali kuwa baadhi ya nchi zilizo hatarini zaidi duniani zinakabiliwa na ushuru wa juu zaidi.
"Ulaya inasimama pamoja - kwa biashara, kwa raia, na kwa Wazungu wote, na tutaendelea kujenga madaraja na wale wote ambao kama sisi wanajali kuhusu biashara ya haki na sheria kama msingi wa ustawi
0 Comments