Na Habari Matukio App, Kibaha
MBIO za Mwenge zimekagua eneo la mradi wa maegesho ya magari makubwa ambao utakapokamilika utaiingizia Halmashauri ya Mji Kibaha kiasi cha shilingi bilioni 3.3 kwa mwaka.
Akikagua na kupata taarifa kwenye mradi huo uliopo Kata ya Misugusugu kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ismail Ussi amesema kuwa hicho ni chanzo kizuri cha mapato kwa Halmashauri hiyo.
Ussi amesema kuwa mradi huo wa maegesho hayo ambayo yatakuwa ya kisasa yataifanya Halmashauri kuongeza mapato yake hivyo kuendelea kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
"Jambo ambalo ni zuri ni kulipa fidia na maendelezo kiasi kikichotengwa ni bilioni 1.8 kwa watu 23 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kimelipwa kwa watu 21 hii inaonyesha kuwa wananchi wanalipwa haki zao na hakuna mtu atakaye kosa haki yake,"amesema Ussi.
Kwa upande wake Mthamini wa Halmashsuri ya Mji Kibaha Patrick Kibwana amesema kuwa mradi huo utakuwa wa shilingi bilioni 23 ikiwa ni mapato ya ndani.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amesema kuwa maegesho hayo yamejengwa jirani na eneo la viwanda la Zegereni hivyo huduma hiyo inahitajika sana.
mwisho.
0 Comments