Header Ads Widget

RC MBEYA ATANGAZA MPANGILIO MJI WA KISASA MBALIZI, MBEYA MJINI.


Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Dkt. Juma Homera, amesema katika mikakati ya Serikali ya Tanzania ya kuimarisha Mipango miji na matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, zaidi ya ekari elfu tano zimepangwa kuendelezwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo makazi na uwekezaji katika maeneo ya Tanganyika Packers, Utengule na Iwambi mkoani Mbeya.

Dkt. Homera amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu utekelezaji wa mradi wa upimaji wa ardhi katika Maeneo ya Utengule na Nsalala mjini Mbalizi yaliyokuwa chini ya Tanganyika Packers na eneo la shirika la utangazaji Tanzania huko Iwambi jijini Mbeya.

Amewaarifu wananchi wa Mkoa wa Mbeya na Wadau wa maendeleo kwa ujumla kuwa mkakati wa kuomba maeneo Serikali kuu ulianza Juni 2024 na unatarajiwa kukamilika Mei 2025 baada ya kukubalika na Serikali kuu juu ya uendelezaji maeneo hayo ili kuleta tija zaidi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

"Napenda kutoa taarifa rasmi kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa upimaji wa ardhi unaoendelea katika Mkoa wetu wa Mbeya. Mradi huu ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuimarisha Mipango miji na matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya wananchi wetu", ameeleza mkuu wa mkoa wa Mbeya Dkt. Juma Zubery Homera.

Aidha ameeleza kuwa mradi huo unatekelezwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, kupitia Mkandarasi ambaye ni Chuo cha Ardhi Morogoro ambapo maeneo hayo kwa eneo la Nsalala Mbalizi ni jumla ya ekari 4855,Utengule Mbalizi ekari 252.39 naTBC Iwambi ekari 169.69.

Mkoa wa Mbeya unashiriki kwenye mradi huo wa uendelezaji maeneo hayo kama sehemu ya juhudi za kitaifa za kuandaa ardhi kwa maendeleo ya kisasa huo tangu ulipoanza rasmi kutekelezwa mwezi Juni 2024, ukitarajiwa kukamilika Mei 2025 ambapo matarajio ya umma na Serikali ni kuona matokeo makubwa na yenye tija katika maeneo lengwa na hatimaye kuchochea kasi ya maendeleo kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI