Header Ads Widget

VITA VYA SUDAN: WANAMGAMBO WA RSF WAKIRI KUDHIBITI KAMBI YA ZAMZAM

 

Kambi ya Zamzam iliyoko karibu na El Fasher inafadhili maelfu ya watu, wanaoishi katika hali ya makali ya njaa

Kufuatia mapigano makali nchini Sudan, wanamgambo wa RSF wamesema wamedhibiti kambi ya wakimbizi ya ZamZam, ambayo imehifadhi watu waliokimbia makwao Darfur Kaskazini.

Mamia ya familia wanaotoroka kambi ya ZamZam wamewasili eneo la Tawila.

Wakati huohuo, Waasi wa RSF wametangaza kuwa wanakaribia kudhibiti kikamilifu eneo la El Fasher, mji muhimu wa Darfur wakiendelea kupigana na wanajeshi wa Sudan.

Mashambulizi mabaya kwenye kambi inayohifadhi mamia kwa maelfu ya watu waliokimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan yameendelea kwa siku ya tatu, wakaazi wameiambia BBC.

Mtu mmoja katika kambi ya Zamzam alielezea hali hiyo kuwa ya "janga" huku mwingine akisema mambo ni "mabaya".

Zaidi ya raia 100, miongoni mwao wakiwa watoto 20 na timu ya madaktari, wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyoanza mwishoni mwa juma lililopita katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan, Umoja wa Mataifa umesema.

Siku ya Jumapili kundi hilo lilisema limechukua udhibiti wa Zamzam lakini likakanusha ripoti za ukatili.

Kambi hizo, Zamzam na Abu Shouk, zinatoa makazi ya muda kwa zaidi ya watu 700,000, ambao wengi wao wanakabiliwa na njaa.

Habari za mashambulizi hayo zinakuja katika mkesha wa kuadhimisha mwaka wa pili wa kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya RSF na jeshi la Sudan.

El-Fasher ni mji mkuu wa mwisho huko Darfur chini ya udhibiti wa jeshi la Sudan na umekuwa ukizingirwa na RSF kwa mwaka mmoja.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI