Na Matukio Daima Media
KAZI ya ushereheshaji (MC) kwenye Sherehe imekuwa ni Moja kati ya kazi zinazowafanya watu wengi kutoboa maisha haraka zaidi japo ubunifu nduni wa washereheshaji hao umekuwa kikwazo.
Idadi kubwa ya ma MC wa zamani wamekuwa wakifanya kazi hiyo kimazoea na kuwa sababu ya kamati za Sherehe mbali mbali kukimbilia kuagiza ma MC toka nje ya mikoa Yao ambao hulipwa pesa kubwa kwa kazi Ile Ile ambayo MC mzawa angeweza kuifanya tena kwa gharama Ndogo na kiwango zaidi.
Kikwazo Kikubwa kwa Ma MC wa kongwe ni mazoea na kutokuwa wabunifu wa kuzalisha Maneno na kwenda kisasa kulingana na Teknolojia ya sasa .
Imekuwa ni kawaida kwa ma MC wa zamani Kila Sherehe mbinu Yao ni hiyo hiyo kuanza kufungua Sherehe Hadi kufunga na hata kucheza ni muziki huo huo Sherehe Zote ukitazama DVD zinafanana .
Kutokana na pendo kubwa la kiubunifu kwenye tasnia hiyo Shan Nicolaus Ngeng’ena ni mmoja wa vijana wachache nchini Tanzania waliobahatika kuibuka na vipaji vingi vinavyojieleza kwa matendo.
Ingawa wengi wanamfahamu kama mwanahabari mahiri aliyepitia vyombo mbalimbali vya habari, kwa sasa Shan anajitambulisha kwa sura mpya kabisa – MC chipukizi mwenye ndoto kubwa ya kuleta mageuzi katika sekta ya burudani na mawasiliano ya hadhara, hususan mkoani Iringa.
Shan alipata elimu yake ya uandishi wa habari katika chuo cha Dodoma Media College, ambako si tu alionyesha umahiri darasani, bali pia alichaguliwa kuwa Rais wa chuo.
Nafasi hiyo ilimfundisha uongozi, mawasiliano na kujituma sifa ambazo zimekuwa nguzo muhimu katika safari yake ya kazi na maisha.
Baada ya chuo alitumia vyema elimu yake kwa kufanya kazi na Dodoma FM na Dodoma TV, kabla ya kupata nafasi adhimu ya kushirikiana na BBC Media Action kupitia kipindi maarufu cha Sanuka.
Ikumbukwe kuwa hii ilikuwa hatua kubwa katika maisha yake ya kiuandishi, ikimfungulia milango ya kufanya kazi Dar es Salaam kupitia EA Radio na EA TV.
Kwa sasa, Shan anasikika kupitia Shamba FM radio pendwa mkoa wa Iringa na maeneo ya Jirani kwa kuwa Jirani na wakulima akitumia sauti yake kuvutia na kuelimisha jamii kwa namna ya kipekee.
Pamoja ya kuwa na historia ndefu katika uandishi wa habari, Shan ameibuka pia kama MC mwenye kipaji cha hali ya juu.
Ingawa amefanya kazi nyingi za U-MC katika harusi, send-off, sherehe za familia na matukio ya kijamii, changamoto kubwa ilikuwa kutokuwa na uwepo wa kudumu kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyomfanya kutotambulika sana katika anga hiyo.
Hata hivyo, leo hii anafungua ukurasa mpya kwa nguvu na msisimko mkubwa zaidi na kushikwa mkono na vyombo vya habari vikubwa hapa nchini kama shamba FM na Matukio Daima Media.
Shani anasema ndoto yake kubadili mwelekeo wa kazi hii kuwa na mvuto zaidi .
“Nimefanya kazi nyingi za U-MC lakini hazikurekodiwa kwa sababu wakati huo sikuwa active kwenye mitandao lakini sasa jamii inipokee rasmi kwenye ukurasa wangu mpya kama Master of Ceremonies, kipaji ninacho,” anasema Shan kwa kujiamini.
Kwani anaamini kuwa U-MC ni sanaa inayohitaji akili kubwa , lugha, ubunifu, uchangamfu na mawasiliano mazuri na hadhira vyote anavyo.
Akiwa na historia ya kufanya kazi na vyombo vikubwa vya habari, anatumia uzoefu huo kuwapa wateja wake huduma za kiwango cha juu iwe ni kwa shughuli rasmi, sherehe za kifamilia au matukio ya kijamii.
Shan anajipambanua kama MC wa kizazi kipya ambaye anakuja na mbinu za kisasa, matumizi ya lugha fasaha, uchekeshaji wa kuvutia na weledi mkubwa wa kuongoza shughuli.
Malengo yake ni kuwa MC maarufu sio tu Iringa, bali Tanzania nzima – akiongoza matukio makubwa kwa nidhamu, ucheshi na umahiri.
Hivyo anawakaribisha watu wote walioko Iringa na nje ya Iringa kumpa nafasi ya kuonesha uwezo wake kwani amefungua njia ya mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii na anaahidi kuwapa wateja wake kile walichokikosa kwa muda mrefu – MC wa kipekee anayejua kazi na anayegusa mioyo ya watu kwa sauti yake na uchezaji wake wa maneno.
Shan Nicolaus Ngeng’ena ni jina jipya lakini lenye uzito mkubwa Kama ulikuwa unatafuta MC mwenye mvuto, nidhamu, ubunifu na uelewa wa hali ya juu wa hadhira basi hujachelewa.
Francis Godwin mkurugenzi wa Matukio Daima Media anasema kama sehemu ya malengo ya Chombo chake kukuza vipaji ameona Uwezo na Nia ya Shan katika kazi hiyo hivyo amejitolea kutangaza bila malipo miezi Mitatu kupitia Matukio Daima Media
Na kuwakaribishe wadau wengine kumtumia Shan kwenye shughuli zao ili kuona Jinsi Sherehe zao zitakavyokuwa na Mageuzi Makubwa na Matukio Daima Tv itakuwa ikirusha kazi hizo .
Iwapo Unahitaji kuwasiliana na MC Shan piga simu 0754026299 au +255765181872
0 Comments