NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMA MWANZA.
Mwalimu wa shule ya Sekondari Nyakabungo Edward Bihemo Mwenye umri wa miaka 43 Mkazi wa mtaa wa Nyamanoro Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza ametapeliwa na mganga wa tiba asilia aliyejulikana Kwa jina la Edward Emmanuel kiasi Cha sh, Mil 12,470.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mtafungwa ameeleza kuwa jeshi la polisi lilimkamata Edward Emmanuel miaka 38 na mmiliki wa nyumba ya kulala wageni Private Lodge Mkazi wa Nyamohongolo Wilaya Ilemela Kwa kosa la kujipatia pesa Kwa njia ya udanganyifu.
Mtafungwa ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo April 18 Mwaka huu kujipatia fedha Kwa njia ya udanganyifu Kwa kumlaghai Edward Bihemo kupitia kazi yake ya uganga wa tiba asilia.
Mtuhumiwa Edward Emmanuel alimweleza Edward Bihemo kuwa ana uwezo wa kuzalisha fedha Kwa njia ya miujiza ambapo mtuhumiwa alichukuwa fedha hizo na kuziweka katika begi lake na kumuamuru mhanga awe anazitolea sadaka mara Kwa mara ili ziweze kuongezeka.
"Aliendelea kutoa sadaka hizo Kwa muda mrefu hadi kufika hatua ya kukosa fedha ya kujikimu na kuamua kwenda Kwa mtuhumiwa Kwa lengo la kuchukua fedha alizowekeza na ndio alipogundua kuwa alikuwa ametapeliwa" Alisema Mtafungwa.
0 Comments