Header Ads Widget

FURAHIKA YAJA NA MPANGO HUU KWA WAFANYAKAZI

Na Matukio DaimaApp 

Wafanyakazi wa Serikali na Sekta binafsi wametakiwa  kuchangamkia fursa ya  kujiunga na Chuo Cha Ufundi  Veta Furahika kwa ajili ya masomo ya jioni kwa kozi mbalimbali 


 Lengo la masomo hayo ya jioni kwa kundi hilo imeelezwa kuwa yanalenga kuwaongezea maarifa yenye tija yatakayoleta ufanisi katika majukumu yao ya kiofisi.

 

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. David Msuya amesema kwamba masomo hayo yatawasaidia waajiriwa kuongeza ufanisi katika utendaji wa majukumu ya kila siku na kuachana na kufanya kazi kwa mazoea na yataendana mahitaji ya sasa.

"Masomo haya ya jioni kwa waajiriwa wa Serikali na Sekta binafsi yataanza Machi 5, 2025 kuanzia saa 11 jioni hadi 1:00 usiku hivyo tunawakaribisha wote kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu," amesema.


Dkt Msuya amezitaja kozi zitakazofundishwa chuoni hapo kwa muda wa jioni kuwa ni Public Administration (Utawala wa Umma), Human Resource Management (HRM), Leadership and  Management pamoja na Project Planning and Management, ambapo kozi zote hizi zitatolewa kwa mwaka mmoja .

Kozi nyengine ni za Fedha na Manunuzi ambapo zinatolewa kwa wiki mbili hadi 12 ambayo ni 'Ethics and Integrity in Public service' itakayotolewa kwa miezi 3, pia itatolewa kozi ya biashara itakayogawanywa katika makundi manne ambayo ni Marketing and Sales, Accounting and Finance, Business administration with Human resources.

Aidha, amesema kuwa chuo hicho, kinatoa fursa sawa kwa watanzania katika kuwaendeleza vipaji vyao na kutoa ujuzi ili waweze kujiajiri badala ya kusubiri ajira za kuajiriwa.

Chuo hicho ambayo kipo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam kimesajiliwa na NACTVET kwa namba REG/NACTVET/1113 kinatoa kozi mbalimbali ikiwemo hoteli, ushonaji, Ufundi magari, ualimu, ambapo kozi zote hizo hutolewa bure kwa vijana waliomaliza darasa la Saba, kidato cha nne na wale waliokatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali ambazo wamekutana nazo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI