Header Ads Widget

MBUNGE MUHONGO AELEZEA FURSA ZA KIUCHUMI ZILIZOPO KATA YA BUGOJI

 


Na Shomari Binda-Musoma 

MBUNGE wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo ameelezea fursa za kiuchumi zilizopo Kata ya Bugoji zinazoweza kuwainua wananchi.

Fursa zilizoelezwa ni pamoja na mikopo ya kilimo,uvuvi na ufugaji kutoka benki za CRDB,NMB,NBC na ile ya asilimia 10 kutoka halmashauri.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara kwenye Kata hiyo aprili 2,2025 kwenye Kijiji cha Bugoji wenye lengo la kusikiliza kero za wananchi n̈a kuzitafutia ufumbuzi na kutanzua mikwamo ya miradi ya vijiji vitatu vya Kata hiyo amesema zipo fursa zikitumiwa uchumi utaimalika kwa wananchi.

Muhongo amesema iwapo wananchi watakuwa na uchumi mzuri wataweza kuchangia shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.

Amesema kilimo cha umwagiliaji kwenye bonde jirani la Bugwema kinaweza kufanyika iwapo wananchi watafatilia mikopo ya uwezeshaji kutoka taasisi za kifedha na halmashauri na ipo miradi midogo midogo ya umwagiliaji kwa kutumia maji ya visima



"Mikopo nafuu  kutoka halmashauri yetu yaani kutoka kwenye 10% ya mapato ya ndani ya ipo na itatusaidia kutuinua kiuchumi.

"Kijiji cha Bugoji shule ya Dan Mapigano sekondari 

 ina maabara moja ya somo la baiolojia misingi ya ujenzi wa maabara nyingine mbili (fizikia na kemia) ipo lakini ujenzi umesimama kwa muda mrefu tukiwa na uchumi mzuri tutachangia",amesema.

Amesema uamuzi wa ujenzi wa maabara 2 za masomo ya sayansi uendelee na saruji mifuko 100 atachangia iwapo ujenzi wa maabara hizo mbili utaendelea.

Mbunge huyo amesema katika suala la afya Kijiji cha Kaburabura kimeamua kujenga zahanati yake na alishafanya harambee na kuchangia na kudai kuwa miradi yote itakayoendelea kutekelezwa nae ataichangia kama alivyoahidi.

Wadau wa maendeleo ya Musoma Vijijini wakiwemo wazaliwa wa vijiji wanakaribishwa kuchangia miradi hiyo husika.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI