Header Ads Widget

MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) MEJA JENERALI RAJABU MABELE AMEWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE UJENZI WA NYUMBA ZA WAGENI BUSTANI YA WANYAMA RUVU JKT

 


MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa nyumba za kulala wageni katika bustani ya wanyama ambayo inasimamiwa na kikosi cha Jeshi 832 Ruvu JKT Kibaha Mlandizi mkoani Pwani na kuwataka kutembelea bustani hiyo kupumzika na kujionea vivutio vya wanyama mbalimbali.


Amesema sababu ya kuanzisha bustani za wanyama kwenye vikosi ni pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato na kutangaza utalii hapa nchini 

Meja Jenerali  Mabele amesema mradi wa bustani ya wanyama mbali ya kuwepo katika kikosi hicho pia ulishaanzishwa kikosi cha Mbweni jijini Dar es salam.

Amesema bustani hiyo ni sehemu ya kutangaza utalii na kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya Royal tour na  kwamba wataendelea kuongeza wanyama ili kuwavutia watalii wa ndani na nje ya nchi.

Mkuu huyo wa Jeshi pia amesema uwepo wa bustani hiyo inawawezesha wananchi wanaoshindwa kwenda mbuga za Mikumi na nyingine hapa nchini kujionea wanyama mbalimbali katika eneo hilo.


"Tutaendelea kuongeza wanyama rafiki katika hii bustani ya wanyama na nyumba hizi za kulala zitawawezesha sasa wanaopata fursa ya kutembelea hapa kupata mapumziko kufurahia utalii wa ndani huku wakipata huduma zote hapa," amesema .

Kamanda wa kikosi cha Ruvu JKT  Kanali Peter Mnyani amesema vijana wanaopatiwa mafunzo katika kikosi hicho wamekuwa wakipata mafunzo kwa vitendo na kujifunza uzalendo na shughuli za kiuchumi.


Mbali ya kuweka jiwe la Msingi Meja Jenerali Rajabu Mabele alifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa kujitolea operesheni miaka 60 ya muungano katika Kikosi cha Jeshi 832 Ruvu JKT .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI