Header Ads Widget

RC DAR ASISISTIZA AMANI MKOANI HUMO, AELEZA MAFANIKIO LUKUKI

 


Na Fatma Ally Matukio DaimaApp

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesisitiza kuwa, licha ya tofauti za itikadi za kisiasa zilizopo, lakini mkoa huo utaendelea kuwa salama kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi, huku akiahidi kila aliejiandikisha mkoani humo atapiga kura kwa amani na utulivu


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo usalama wa Mkoa, kasi ya ulipaji wa kodi, maboresho ya miundombinu ya barabara pamoja na nafasi ya mkoa kuelekea uchaguzi mkuu pamoja na jumbe zinazozagaa juu mafuriko na hatua zilizochukuliwa na Serikali.


Aidha, amewataka wananchi wa mkoa huo waliojiandikisha kwenye  daftari la kudumu la mpiga kura, siku ya Uchaguzi kujitokeza kupiga kura kwani kutakuwa na mazingira salama.



Hata hivyo amewataka wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu kwani Jeshi la polisi litafika kila penye viashiria vya uvunjifu wa amani ili kuhakikisha mkoa huo unakua na amani.


"Tunafahamu kuelekea Uchaguzi wapo watu wanaweza kuwa na

 malalamiko, hivyo wanatakiwa kufuata taratibu na kufikisha malalamiko yao kwa mamlaka husika. Niwahakikishie wafanyabiashara kuanzia sasa hadi Uchaguzi Mkuu hakutakuwa na vurugu,".


Akizungumzia kuhusu miundombinu mkoani humo, RC Chalamila amesema katika kuboresha miundombinu Serikali imeanza ujenzi wa daraja la jangwani ambapo mkandarasi ameanza ujenzi wa karakana ya kuhifadhia vifaa vyake kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa uzenzi huo.


"Nimeona kuna jumbe zinazunguka kwenye mitandao ya kijamii ikiashiria kuwa kutakuwa na vurugu kwenye Mkoa huu. Nataka niwahakikishie hakutakuwa na vurugu yoyote, hakuna hata mmoja ambaye ataweza kuvuruga Amani ya Nchi," amesema RC Chalamila na kuongeza,


Hivyo amesema mkandarasi yupo kazini ambapo  amewataka wananchi kutokuwa na shaka juu ya ujenzi huo ambao unakwenda kuwa suluhisho la mafuriko eneo hilo.


Sambamba na hilo RC Chalamila amezungumzia mpango wa ujenzi wa barabara katika Mkoa huo kupitia mradi wa DMDP ambapo amesema wakandarasi wengi wameshaingia kazini na amewahakikishia wananchi kuwa barabara ambazo bado ujenzi haujaanza ndani ya muda mfupi kazi itaanza pia amesisitiza juu ya mpango wa serikali kuimarisha usafiri wa mwendokasi kupitia wawekezaji binafsi.


Vilevile kupitia mkutano huo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake kuutaarifu umma kupitia vyombo vya habari Mkuu wa Mkoa huo amezungumzia mpango wa biashara saa 24 na kusisitiza kuwa uwepo wa bandari, uwanja wa ndege wa kimataifa,kituo cha mabasi cha magufuli, umeme na soko lakimataifa la kariakoo ni nyenzo muhimu kufikia lengo la biashara saa 24

RC Chalamila amewatakia Kheri ya Pasaka wakristo wote na wakazi wa Dar es Salaam kwa ujumla kusherekea kwa Amani na Utulivu Jeshi la polisi lipo kazini saa 24. Pia amemtangaza Mr Pimbi na wenzake kuanzia leo ni mabarozi wa Mkoa huo wa kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita katika Mkoa huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI